. Jenerali Mella, Kamanda wa Jeshi la UNAMID akibadilisha mawazo na Balozi Mwinyi, ambapo pamoja na mambo mengine, amesema wanajeshi kutoka JWTZ ambao ni sehemu ya UNAMID wameendelea kuonesha weledi na kujituma kwa hali ya juu katika eneo la ulinzi wa amani, ulinzi wa raia na usimamiaji wa misaada ya kibinadamu. Akasema kutokana na mapingano ya kikabili yanajitokeza mara kwa mara, na kuwa sehemu kubwa ya mapigano hayo yamekuwa yakitokea katika maeneo zilipo kambi za wanajeshi kutoka Tanzania, wanajeshi wetu wamejikuta wakilazimika kutoa huduma mbalimbali zikiwamo za kuwazalisha wanawake waja wazito. Utoaji wa huduma hiyo ya uzazi salama nje ya mamlaka yao imewafanya wazazi waliojifungua kuwapatia majina ya kitanzania watoto wao, kama shukrani yao kwa madaktari hao wa kitanzania kwa kuokoa maisha yao na ya watoto wao. Kushoto kwa Jenerali Mella, ni Luteni Kanali, Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu
. Luteni Jenerali Paul Mella, Kamanda wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo yake na Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa ( hayupo pichani). Jenerali Mella alifika katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kufuatia ziara yake ya kikazi ya siku tatu katika Umoja wa Mataifa ambapo alikuwa na mazungumzo na Wakuu mbalimbali wa UN. Akielezea tathmini yake ya miezi nane kama Kamanda wa UNAMID Jenerali Mella anasema njia pekee ya kupatikana kwa amani ya kudumu katika jimbo la Darfur ni kwa pande zinazopingana kukaa katika meza ya mazungumzo na kumaliza tofauti zao
Na
Mwandishi Maalum
Kamanda
wa Jeshi la Mseto la Umoja wa Afrika na
Umoja wa Mataifa katika Darfur ( UNAMID) Luteni Jenerali Paul Mella, amesema, mazungumzo yatakayozihusisha pande zote
zinazopingana katika mgogoro na
machafuko yanayoendelea katika Jimbo la Darfur
ndiyo suluhu pekee inayoweza
kurejesha hali ya Amani, usalama na
utulivu katika jimbo hilo.
Jenerali
Mella, ameyasema hayo wakati
alipokuwa akibadilishana mawazo na
Balozi Ramadhani Mwinyi, Naibu
Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa
Mataifa, wakati Jenerali Mella alipoutembelea
Uwakilishi wa Kudumu.
Kamanda
wa Jeshi la UNAMID alikuwa hapa Makao Makuu ya Umoja wa
Mataifa kwa ziara ya kikazi ya siku tatu,
ambapo alikutana na kufanya
mazungumzo na Viongozi mbalimbali
wa Umoja wa Mataifa.
“Katika kipindi changu za miezi nane sasa kama
kamanda wa UNAMID yapo mambo mengi ambayo nimejifunza zikiwamo pia changamoto mbalimbali katika eneo zima la
ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur. Kubwa la msingi ambalo nimejifunza, ni kwamba, Amani ya
kudumu haiwezi kurejea katika jimbo la
Darfur kama pande zote zinazopingana
hazitaweza kukaa katika meza moja
na kufanya mazungumzo” anasema
Jenerali Mella.
Na
kuongeza “ kwa tathmini yangu , wanajeshi wanaounda UNAMID wapo pale kulinda Amani, kutoa ulinzi kwa wananchi na kusaidia usambazaji
wa misaada ya kibinadamu. Lakini kwa
kweli, hakuna Amani ya kulinda, kwa
sababu moja kubwa, nayo ni kwamba pande
zinazopingana hazijafikia makubaliano
ya kusitisha mapigano na kurejea katika
meza ya mazungumzo.”
Akielezea
zaidi tathmini yake katika kipindi hicho ya miezi nane ambapo anaongoza zaidi ya walinzi wa Amani (wanajeshi)14,379 wanaounda UNAMID. Jenerali Mella, anaeleza kwamba, tangu achukue uongozi huo, kumekuwapo na
mabadiliko katika mwenendo mzima wa mapigano katika jimbo hilo.
“
Changamoto kubwa niliyokumbana nayo ni
kuwa katika miezi hiyo nane ya uongozi
wangu, mwenendo mzima wa machafuko au mapingano umebadilika na kujikita zaidi katika mapigano ya kikabila” anabainisha na kuongeza.
“Mapigano
hayo ya kikabili na ambayo chimbuko lake ni kugombea raslimali zikiwamo
dhahabu mafuta na malisho, yamepelekea kuwapo kwa wimbi kubwa la
wakimbizi wa ndani.
Jenerali
Mella anasema, sehemu kubwa ya mapingano
hiyo baina ya makabila yalikuwa yanatokea
karibu na maeneo zilipo kambi zetu kwa
maana ya wanajeshi kutoka Jeshi la wananchi wa Tanzania ( JWTZ). Ninafarijika
sana kueleza kwamba wanajeshi wetu wameonyesha
weledi na uhodari wa hali ya juu kwanza kwa kutoa ulinzi kwa raia waliokuwa
wakikimbia machafuko na pili kuwapatia misaada ya kibinadamu zikiwamo huduma za
afya”.
“Ni
katika kipindi hicho cha mapigano ambapo licha ya utoaji wa huduma za kibinadamu kwa wakimbizi hao, walinzi wetu wa Amani ( JWTZ), walijikuta
wakilazimika kutoa huduma za dharura kwa akina mama wajawazito zaidi ya saba
waliojifungua salama watoto wao katika kambi zetu”.
“ Huduma
hii ya kuwasaidia akina mama wajawazito
kujifungua salama watoto wao, kuliwafanya
wazazi wale kuwapa watoto wao majina ya kitanzania kama shukrani yao
kwa msaada na huduma
nzuri waliyopatiwa na madaktari
wa kitanzania katika kipindi hicho kigumu. Kuna watoto wenye majina ya
kitanzania” anasema Jenerali Mella kwa
furaha.
Kwa
upande wake, Balozi Mwinyi ameshukuru
Kamanda wa Jeshi la UNAMID kwa kutenga muda wake na kufika
Uwakilishi wa Kudumu. Akashukuru pia kwa maelezo yake ya kina kuhusu hali ilivyo katika jimbo hilo la Darfur na mchango mzima wa walinzi wa Amani.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, ina kikosi UNAMID
kinacho kalia maeneo matatu
ambayo ni Khor Abeche, Menawashe na Shangil Tobaya.
Tanzania inakuwa nchi ya tatu kongoza UNAMID , nchi nyingine ambazo zimewahi
kuongoza ni Nigeria na Rwanda.
1 comment:
Kwanini uwanja unajengwa sehemu hiyo hiyo, wa develop sehemu nyengine.
Post a Comment