Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai amkaribisha nyumbani kwake Mhe. Fredrick Sumaye na kuongea na Watanzania waliokutana nyumbani kwa Mhe. Mjenga kwa chakula cha jioni kwa ajili ya siku kuu ya Muungano. Maadhimisho ya sherehe za Muungano yalifanyika tarehe 14 Aprili 2014 katika hotel ya Le Meridien. Sherehe hizo zilihudhuriwa na Mhe. Lazaro Nyalandu na Mhe. Rashid Fahad, Waziri wa Mazingira na Maji wa Serikali ya Muungano wa Falme za Kiarabu (UAE).
Mheshimiwa Sumaye akimkabidhi cheti cha Utambuzi na Shukuran kwa BwanaRajen Kilachand, Rais wa Kampuni ya Dodsal inayowekeza Tanzania kwenye
sekta ya mafuta na madini, kwa hisani ya mchango wake mkubwa wa
kufanikisha sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano,
zilizofanyika hapa Dubai tarehe 14 Aprili, 2014.Wengine katika picha
hizo ni Mhe. Omar Mjenga, Balozi Mdogo, na Ndugu Mohamed Sharif (
Mwenye suti na tai) Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio UAE,
Mama Balozi Mdogo Asha Mjenga (Mwenye Kilemba kichwani) na Mama
Kilachand (mwenye suti nyeusi). Ile picha nyingine, wakiwa katika
mazungumzo katika Ukumbi wa Majlis nyumbani kwa Mhe. Balozi Mdogo.
Picha ya pamoja
Watanzania waishio UAE wakijumuika nyumbani kwa Mhe.Balozi Mdogo kwa ajili ya chakula cha jioni.
No comments:
Post a Comment