Mjengo
wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo Mbezi
Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam umeingia kwenye lawama kufuatia madai
kwamba, unatumika kwa kutapeli watu wanaotaka kununua nyumba maeneo hayo.
Mjengo wa staa wa filamu za Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ uliopo
Mbezi Temboni-Salanga jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa
chanzo chetu ambacho kina makazi jirani na n
yumba hiyo, baadhi ya watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
yumba hiyo, baadhi ya watu wanaojiita madalali wamekuwa wakiwapeleka wateja kwa siri kwenye nyumba hiyo ambayo haijaisha na kusema inauzwa na Lulu mwenyewe.
MCHEZO ULIVYO“Baadhi ya madalali feki wamekuwa wakiwaleta wateja wanaotaka kununua nyumba maeneo haya. Wakifika wanasema Lulu anaiuza, wakiwa wameshaiona wanatoa fedha za usumbufu au za kuwapoza wasipeleke watej wengine na kutoa namba feki ya Lulu ili mteja ampigie.
“Wapo wateja
walishanifuata na kusema wanampigia Lulu hapatikani, lakini waliponionesha namba
yenyewe si ya Lulu.
“Siku moja mteja
mmoja aliletwa na dalali kuiona nyumba, akaipenda, akampa dalali shilingi
300,000 za kumfanya asipeleke wateja wengine, akampigia Lulu hakupatikana.
Alipokuja kwangu nikaiangalia namba hiyo ilisajiliwa kwa jina la Mwanahamis nani
sijui,” kilisema chanzo hicho.
MAPAPARAZI WAJIFANYA WATEJA, MADALALI
WASHTUKA
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na Mambeze ‘Mchopa’.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, mapaparazi wetu walijifanya wateja wa kuinunua nyumba hiyo na kwenda kukutana na watu wawili waliodaiwa kuwa ndiyo madalali, Kitwana na Mambeze ‘Mchopa’.
Baada ya
mazungumzo, madalali hao walidai kuwa, funguo za kuingia ndani ya nyumba hiyo
anazo mama Lulu (Lucresia Karugila) na alisema angefika siku hiyo saa kumi jioni
na kuwataka mapaparazi kurudi muda huo.
Wakati mapaparazi
wetu wanaondoka, dalali mmoja alisema: “Nyie kama mmekuja kututega mmeliwa
wenyewe, hapa hakuna mtoto wa kijijini. Wanaokuja hapa kutaka nyumba
wanajulikana, nyie mmetumwa.”
LULU ALISHAFIKA, HAJUI KITU
Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya kuiuza!
Sosi mwingine alisema hivi karibuni alimuona Lulu akifika eneo hilo kwa ajili ya kuangalia nyumba hiyo ambayo imesimama ujenzi lakini hakuweka wazi kama alikuwa na nia ya kuiuza!
“Mimi mara ya
mwisho nilimuona Lulu eneo hili na gari lake, naona alikuja kuangalia nyumba
inaendeleaje na usalama pia. Mambo ya kuwa anaiuza hata siyajui ingawa kweli
hata mimi nimekuwa nikiwaona watu wakija,” alisema sosi huyo ambaye hakutaka
jina lake lichorwe gazetini.
Juzi, gazeti hili
lilimsaka Lulu kwa njia ya simu kwa ajili ya kumuuliza kuhusu suala hilo ambapo,
awali aling’aka, akasema
“Wewe ndiyo
unaniambia kusema ukweli, sijui chochote. Naomba mnipe habari kwa upana ilivyo
maana nyie waandishi mara nyingi mnakuaga wa kwanza kujua habari kuliko
mhusika.”
Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu, kama unaiuza. Nilichokwambia ndicho.
Amani: Wewe Lulu sema ukweli tu, kama unaiuza. Nilichokwambia ndicho.
Lulu: Kweli mimi
siiuzi nyumba yangu wala sina wazo. Huyo aliyewapa habari awape kwa undani ili
nijue.”
>>>Amani
No comments:
Post a Comment