Advertisements

Friday, April 18, 2014

MSIKILIZE TUNDU LISSU AKIJIBU TUHUMA ZA KUMZALILISHA BABA WA TAIFA MWL. JULIUS NYERERE

5 comments:

Anonymous said...

Hakika anajua anachokiongea. Hili suala la muungano limefichwa fichwa sana lakini wakielezwa ukweli wanakuja juu. Nashukuru DJ Luke kwa kuweka hii clip ili watu waone halafu kwa sababu tunao uwezo wa kufikiri tuchambue kipi kizuri kuliko kuweka propaganda za chama cha Mapinduzi kama anavyofanya michuzi blog na kuminya uhuru wa maoni kitu ambacho kinakandamiza demokrasia. Binafsi natatazika sana ninapoona rais Kikwete hana mamlaka ya kufanya lolote kule Zanzibar, hapigiwi mizinga 21, hagawanyi wilaya/mikoa, kwenye sherehe huko ZNZ anapanga mstari kama wageni wengine nk.nk. Sasa akiwa rais wa muungano si pamoja na Zanzibar? Sasa huyo rais wa ZNZ aweje ni amiri jeshi mkuu wa vikosi vya Zanzibar? Kama ni hivyo basi ZnZ ni nchi iyojitegemea, na kama ni nchi inayojitegemea sasa inapata mgao wa 4.5% wa fedha kutoka jamhuri ya muungano kwa sababu gani? Tunataka mambo yawe wazi, binafsi siwakilishi na si mwanachama wa chama chochote cha siasa na sikuwahi kuwa, ila kama mtanzania mzalendo natatizwa sana na hii discrepancy...sielewi kabisa. Kuwe na suluhisho ambalo litarekebisha katiba ya ZNZ au kila nchi ichukue utaratibu wake na huo unaoitwa muungano usiwepo. We need to be bold to solve our problems. Mpaka lini tutaendelea kudanganyana? Hizi kero zitaendelea hadi lini?

Anonymous said...

HE IS THE ONE! TINDU LISU FOR PRESIDENT. WE WAITED FOR SO LONG FINALLY GOD SENT YOU. ITS TIME FOR TANZANIA TO MOVE FORWARD

Anonymous said...

lagujuu mtakaa hivyo hivyo wadanganyika mnataka mpigiwe mizinga nyinyi sijui mgawe mikoa kwani zanzibar ni mkoa, zanzibar ni nchi si mkoa na ilikuwa na inshallah itakuwa nchi sasa mnataka njama zenu za kuiuwa zanzibar biizni lillahi hamtofanikiwa amin amin amin

ujanja wa nyerere kutaka kumeza zanzibar ulishindikana na ndo maana hakuna hati ya karume sasa mnataka kupigiwa mizinga na kugawa mikoa biizni lillahi hamtofanikiwa

hasid idhaa hasad watanganyika wote na mahafidhina wenu tukipata nchi yetu njoeni muwachukuwe huko kwenu tanganyika

Anonymous said...

disrepancy hii inayo nyinyi huko kwenu tanganyika hatutaki sisi muungano kwa nini mnatulazimisha kuunga ndo muiuwe nchi yetu kwa lipi hiyo 4.5% kwani tunapata si mnachukuwa nyinyi tena kwa dhulma zenu.

dj luke ahsante kwa kuweka hii clips na waliokwenda shule wataona faida yake na hatoiuwa nchi yetu ZANZIBAR ilikuwa nchi na itaendelea kuwa nchi si MKOA ULE

Anonymous said...

dj luke anafanya kistaarabu kwa vile yuko marekani yule mndengereko wa rufiji yuko bongo ndo maana yuko ccm ukiwa ccm unapata ugari wako ndo maana michuzi yeye hatoacha kuweka mambo ya ccm na ndo maana na mimi nimeacha kuingia katika blog yake long long long long time ago ukiweka comment zako ukikosoa ccm haweki ameshakunywa maji ya bendera ya ccm na anapata ugari wake achana naye

i hope dj luke hatokuwa hivyo