ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 15, 2014

Mwanamuziki maarufu akamatwa Rwanda


Wapiganaji wa FDLR
Mwanamuziki mashuhuri nchini Rwanda pamoja na mwanahabari mmoja wamekamatwa kwa tuhuma za kuwa na uhusiano na kundi la upinzani pamoja na kushirikiana na waasi.
Kwa mujibu wa polisi ,Cassien Ntamuhanga ambaye ni mkurugenzi wa, kituo cha redio ya kikristo alikamatwa Jumatatu huku mwanamuziki Kizito Mihigo akikamatwa mnamo Ijumaa.
Wawili hao wanatuhumiwa kuwa na uhusiano na chama cha kisiasa cha (RNC) kilicho na makao yake nchini Afrika Kusini.
Pia wanadaiwa kuwa na uhusiano na waasi wa
Hutu walio katika nchi jirani ya DRC.
Chama cha RNC kiliundwa na Patrick Karegeya,aliyepatikana akiwa amefariki katika hoteli moja nchini Afrika Kusini mapema mwaka huu.
Washirika wake pamoja na familia yake wanalaumu serikali ya Rwanda, kwa mauaji yake madai ambayo Rwanda imekanusha vikali.
Polisi wadai kuwa wawili hao pamoja na aliyekuwa mwanajeshi Jean Paul Dukuzumuremyi, walipanga mashambulizi ya kigaidi kwa lengo la kupindua serikali na kuwaua maafisa wa serikali na pia kuchochea ghasia.
Wanadaiwa kushirikiana na waasi wa FDLR ambao baadhi ya viongozi wao walishiriki katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu 800,000 wa kabila la Tutsi na wahutu wenye msimamo wa kadri waliuawa.
Inaarifiwa bwana Mihigo alikuwa na uhusiano wa karibu na chama tawala cha (RPF),na kwamba kukamatwa kwake kumewashangaza wengi.
Rais Paul Kagame aliingia mamlakani punde baada ya mauaji ya kimbari kumalizika.
Wengi wamemsifu kwa kukuza uchumi wa nchi hiyo huku baadhi wakimlaumu kwa kukandamiza uhuru wa watu kujieleza.
BBC

No comments: