Daktari
Luvanda kutoka hospitali ya wilaya ya Makete akionesha majeraha ya
kichwa cha mwili wa marehemu yanayohisiwa kupelekea kifo chake.
Polisi
kutoka kituo cha Tandala na Makete wilayani wakichukua taarifa za
mauaji hayo kwenye shamba ulipokutwa mwili wa marehemu.
Askari
akizungumza na wananchi waliofika eneo la tukio na kuwaonya kuacha
tabia ya kujichukulia sheria mikononi pamoja na kushirikiana na jeshi
hilo kuwapata watuhumiwa wa mauaji hayo.
Mkazi wa kijiji cha Masisiwe kata ya Ukwama Wilayani Makete Mkoani Njombe
amefariki Dunia baada ya kupigwa na kitu chenye ncha kali kichwani na mguuni na mtu/watu
wasiojulikana mwishoni mwa wiki iliyopita
Akithibitisha
kutokea
kwa tukio hilo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya, Mrakibu mwandamizi
wa Polisi ambaye pia ni afisa upelelezi Wilaya ya Makete Bw.Gozbert
Komba
amesema walipokea taarifa ya mauaji hayo kutoka kwa uongozi wa kijiji
hicho na
kumtaja marehemu kuwa ni Masori Sanga(60) mkazi wa kijiji cha Masisiwe
Kata ya
Ukwama Wilayani Makete
Bw.
Komba
amesema kuwa marehemu huyo aliuawa usiku wa kuamikia Ijumaa wiki
iliyopita na
watu wasiojulikana kwa imani za kishirikina kwa kuwa marehemu alikuwa
mzee na pia kwa mujibu wa maelezo ya mashuhuda wa tukio hilo waliohojiwa
na polisi
Pia
amesema mpaka sasa Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kwa ajili ya kuhakikisha
wahusika wote wa tukio hilo wanakamatwa kwani kitendo walichokifanya ni cha
kinyama na baada ya tukio hilo muuaji/wauaji
hao walitokomea kusiko julikana
Bw.Komba
amekemea vikali suala la wananchi
kujichukulia sheria mkononi wilayani hapo na kuwaomba wananchi wasiwe na
tabia hizo za kuwaua wazee kwa imani za kishirikina na kuwataka watii sheria bila
shuruti ili kuishi kwa Amani katika wilaya yao na nchini kwa ujumla
Mwili
wa marehemu ulikutwa kwenye shamba la mahindi ukiwa na majeraha sehemu
za kichwani na mguuni ambayo yanadhaniwa kusababisha kifo chake, baada
ya watu kupita eneo hilo na kuukuta mwili huo
katika
kipindi cha hivi karibuni wilayani Makete kumekuwa na matukio ya mauaji
kutokana na tuhuma mbalimbali ikiwemo wivu wa kimapenzi na imani za
kishirikina jambo linalotia doa wilaya hiyo kutokana na ongezeko la watu
kuchukua sheria mikononi kwa kuwaua watuhumiwa wa matukio mbalimbali
No comments:
Post a Comment