Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka Wizara ya Ushirikiano wa
Afrika Mashariki Bi. Vedastina Justinian akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu Mradi wa Vituo vya Utoaji Huduma
kwa Pamoja Mipakani (One Stop Border Posts) unaolenga kurahisisha
taratibu za forodha, uhamiaji, usimamizi wa ubora wa bidhaa, ulinzi na
usalama. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi Miundombinu ya Kiuchumi Mhandisi
Abdillah Mataka na kulia ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Bw.
Frank Mvungi.
PICHA ZOTE NA FATMA SALUM
……………………………………………………………………………………………………
Na Frank Mvungi-Maelezo
Serikali
imejipanga kukamilisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja Mipakani
(One Stop Border Posts-OSBP) vitakavyosaidia kurahisisha taratibu za
forodha,uhamiaji,Usimamizi wa ubora wa bidhaa na huduma ,usalama na
ulinzi kwa kutoa huduma hizi upande mmoja wa mpaka.
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Vedastinian Jastinian wakati wa mkutano
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akieleza
faida za vituo hivyo, Vedastinian amesema vitaondoa urasimu uliokuwepo
awali na kuharakisha huduma na kwa wananchi wa nchi wanachama wakati
wanapotaka kusafirisha bidhaa kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Alisema
Kituo cha kwanza ni kile cha Holili ambacho kimekamilika na
kimekabidhiwa kwa mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) ambao ndio
waendeshaji wa vituo hivyo hapa nchini ambapo mradi huu unatarajiwa
kukamilika mwezi Mei 2014.
Alifafanua
kuwa katika mipaka ya Sirari/Isebania unazitenganisha Tanzania na Kenya
na kwa upande wa Mkoa wa Mara mpaka wa Mutukula unazitanganisha
Tanzania na Uganda.
Vedastinian
alivitaja vituo vingine kuwa ni Namanga cha Arusha,Kabanga/Kobero
kilichopo mpakani mwa Tanzania na Burundi unatarajiwa kukamilika mapema
mwezi novemba 2014.
Alitaja
vituo vingine ni Horohoro Mkoani Tanga na Lungalunga upande wa nchi ya
Kenya ambapo ujenzi wake unatarajia kukamilika mapema mwaka huu.
Mradi
huo unatekelezwa baada ya kutungwa sheria ya jumuiya ya Afrika
Mashariki ya kuanzisha vituo vya utoaji wa huduma kwa pamoja mipakani
(OSBP) Katika nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
Sheria iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na Iko katika hatua za mwisho za kuidhinishwa na Wakuu wan chi wanachama.
No comments:
Post a Comment