Advertisements

Friday, April 18, 2014

TANGAZO LA KUHAMA OFISI

SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
WAZEE WA KAZI
GOOD NEWS!

Ndugu zanguni,

Tunapenda kuwapa habari njema watu wote kuwa kuanzia tarehe 01/05/2014 Kampuni yetu inayomilikiwa na Watanzania waishio UK, inahamishia ofisi zake ndani ya bandari kubwa kuliko zote za kusafirisha magari UK , PORT OF TILBURY.

Sisi tutakuwa weusi wa kwanza kabisa kupewa ofisi ndani ya hii bandari na hivyo majina yetu kuingia kwenye historia. Na serikali imetukubali baada ya kuona jinsi tulivyoweza kujibeba kutoka kwenye kiosk mpaka tulipo

Mkumbuke Serengeti ilianzishwa kwa mtaji wa £1,800 tu.

Tumepewa mkataba wa miaka kumi na tunaweza ku renew baada ya hapo kama bado tutakuwa tunataka kuendelea na biashara ndani ya bandari

Tumechukua Yard yenye ukubwa wa ekari mbili na ofisi yenye ukubwa wa 2,500sq ft.

Hii itatusaidia kuboresha huduma zetu kwa sababu tuna mpango wa kukodi meli ya saizi ya kati ili magari yetu yote na makontena tuwe tunasafirisha wenyewe na pia kusafirisha magari na makontena ya makampuni mengine pia.

Pia usalama wa mali za wateja ni maximum kwa sababu kuna zaidi ya camera 5,000, kituo cha polisi ni hatua mia tatu tu kutoka kwetu, police patrol ni 27/7 

Yard /ofisi zetu zitakuwa OPPOSITE BERTH 31, BESIDE HYUNDAI TERMINAL

Tukiishakamilisha mkataba wa kukodi meli tutatoa punguzo kubwa kwa usafirishaji wa magari kwa asilimia 40% ili kurahisisha watu kuweza kuagiza magari yao toka UK kwa bei nafuu. Pia tutakuwa tunatoa free storage kwa magari na free loading.

Kama kuna mtu ana kitu au mzigo ndani ya ofisi zetu za sasa tunaomba aje achukue sababu hatutahama na mzigo wa mtu

Wote mnakaribishwa.

CHRIS LUKOSI

Managing Director

SERENGETI FREIGHT
WE ARE OPEN ON SATURDAY 10:00-18:00HRS
WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
Tupigie kwa namba hizo hapo chini au  tutumie email tafadhali

CHRIS LUKOSI +44 (0) 790 38 28 119 OR  +44 (0) 7404 27 96 33
SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243

2 comments:

Anonymous said...

Safi sana wazee wa kazi nawapongezeni sana, I wish kama Mzee Haji wa Rodgers Export angekuwa hivo, jamaa huku US ni MUONGO!! Ha deliver anachokisema, mizigo yetu huchelewa sana, na Dj Luke nashangaa sana hukutoa comment zote tulizoandika kuhusu huyu jamaa usibanie!! Lazima watu wajue ukweli kuhusu Haji.

Anonymous said...

Duh huyu jamaa ni kweli ana upeo mdogo sana ki elimu biashara na rangi ya ngozi yako imehusuana wapi mimi sidhani kama hao waliokukodisha ofisi walikuangalia kwanza rangi ya ngozi yako (NYEUSI) sasa sijuwi historia gani unayotaka kuweka ushauri wa bure Mr Lukosi ondosha mawazo ya ukoloni mambo leo kwenye kichwa chako.

Na huyu Hassan kwani bado yupo kwako??? si amefunguwa kampuni yake mwenyewe au ndio njia moja ya kuvutia wateja. Kuwa mkweli, tanuka kimawazo, jivunie who you are kuna siku utafika.