Advertisements

Thursday, April 17, 2014

WANANDIGA 16 WACHAGULIWA MABORESHO YA TAIFA STARS TUKUYU

WACHEZAJI 16 kati ya 34 wa kikosi cha Maboresho ya Timu ya Taifa (Taifa stars) wamechaguliwa kutoka kwenye kambi iliyokuwa ikifanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ualimu Tukuyu Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya .
Kikosi hicho kimetangazwa leo jijini Mbeya na Kocha Msaidizi, Salum Mayanga, aliyekuwa na timu hiyo katika Mkutano na waandishi wa Habari uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Hill View iliyopo mjini humo.
Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni Mlinda mlango Benedict Tinoko Mlekwa kutoka Mara.

Walinzi wa kati: Emma Namwondo Simwanda kutoka Temeke na Joram Nason Mgeveja kutoka Iringa.

Walinzi pembeni : Omari Ally Kindamba kutoka Temeke, Edward Peter Mayunga kutoka Kaskazini Pemba na Shirazy Abdallah Sozigwa kutoka Ilala,viongo wa Ulinzi ni Yusufu Suleiman Mlipili na Said Juma Ally kutoka Mjini Magharibi.

Viungo Washambuliaji: Abubakar Ally Mohamed kutoka Kusini Unguja na Hashimu Ramadhani Magona kutoka Shinyanga, na Viungo wa pembeni ni Omari Athumani Nyenje kutoka Mtwara na Chunga Said Zito kutoka Manyara.

Washambuliaji: Mohammed Seif Said kutoka Kusini Pemba, Ayubu Kassim Lipati kutoka Ilala, Abdurahman Othman Ally kutoka Mjini Magharibi na Paul Michael Bundara kutoka Ilala.

Madadi aliongeza kuwa katika kikosi hicho pia wamechaguliwa wachezaji wawili waliojiunga na Timu ya Taifa ya wenye umri chini ya Miaka 20 ambao ni Mbwana Mshindo Musa kutoka Tanga na Bayaga Atanas Fabian kutoka Mbeya.

Aidha Kocha huyo alisema wachezaji wengine walioachwa wataendelea kuwa kwenye uangalizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu(TFF) kwa sababu mpango wa maboresho ya timu ya Taifa ni endelevu.

Alisema Kambi ya timu hiyo ilianza Machi 22, Mwaka huu na kuhitimishwa Aprili 17, mwaka huu kwa awamu ya kwanza ambapo wachezaji hao watajiunga na kikosi cha Timu ya Taifa cha Awali kwa ajili ya maezo ya mechi ya Kirafiki kisha watarudi tena wilayani Rungwe kwa ajili ya Kambi ya awamu ya Pili.

No comments: