ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 14, 2014

YALIYOJIRI KATIKA MSIBA WA MZEE MUHIDIN MAALIM GURUMO NYUMBANI KWAKE LEO


Sehemu ya Waombolezaji wa Msiba wa nguli wa Muziki wa Dansi hapa nchini na aliekuwa kiongozi wa Bendi ya Msondo Ngoma,Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo wakiwa nyumbani kwake Mabibo (Tabata Makuburi),leo.Shughuli zote za Mazishi zinaendelea nyumbani hapo.Tarati bu za Mazishi zimefanyika,yatafanyika kesho Aprili 15,2014 kwenye Makaburi yaliopo kwenye kijiji cha Masaki,Kisarawe mkoani Pwania.
 Mmoja wa wanamuziki wa zamani na aliewahi kufanya kazi Pamoja na Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo,Mzee Shaaban Dede (wa pili kushoto) akiwa ni miongoni mwa waombolezaji waliofika kwenye msiba huo.
Sehemu ya Waombolezaji wakiwa msibani hapo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA),Godfrey Mngereza (katikati) akijadiliana jambo na Rais Shirikisho la Muzini Tanzania,Ado November (kushoto) pamoja na Mwanamuziki na mpiga Keyboard mahiri nchini,Abdul Salvador a.k.a Father Kidevu juu ya taratibu mbali mbali za Msiba wa Mzee Muhidin Maalim Gurumo,nyumbani kwake Mabibo jijini Dar.
Waombolezaji wakiwa msibani.
Wanamuziki wa Bendi ya Kilimanjaro Band wazee wa Njenje,John Kitime na Mohamed Mrisho wakibadilishana mawazo walipokutana kwenye Msiba wa Mzee Muhidin Maalim Gurumo,nyumbani kwake Mabibo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Wamamuziki waliowahi kufanya kazi na Mzee Gurumo wakisabahiana wakati walipowasili msibani hapo leo.
Kamati ya Mazishi ya Mzee Muhidin Maalim Gurumo ikiwa imekaa kujadiliana maswala mbali mbali.
Mjane wa Marehemu Mzee Muhidin Maalim Gurumo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya maisha yake na Marehemu mumewe.
Wadau wa Muziki.
Mpiga Solo wa Bendi ya Msondo,Ridhiwan Pangamawe akiwa ni mwenye majonzi kwa kuondokewa na Kiongozi wake.
Mzee King Kikii na wadau.
Kiongozi wa Bendi ya Twanga Pepeta,Asha Baraka akiambatana na wanamuziki wake wakiwasili msibani hapo.
Wakisabahiana.
Mzee King Kikii,Rashid Pembe na Abdul Salvador wakiwajadiliana mambo kadha wa kadha juu na namna walivyomkumbuka Mzee Muhidin Maalim Gurumo.
PICHA NA OTMAN MICHUZI

No comments: