Advertisements

Saturday, April 19, 2014

YANGA IMEKULA KWAO KAMA WALIKUWA NA NDOTO YA KURUDISHA BAO 5 MWAKA HUU NDIYO ULIKUWA WAO KUTOKANA NA UBORA WA TIMU YAO.

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam

HATIMAYE safari ya mechi 26 za ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014 imemalizika leo kwa timu zote 14 kushuka uwanjani katika miji tofauti nchini.
Yanga waliovuliwa ubingwa na Azam fc walikuwa wenyeji wa watani zao wa jadi, wekundu wa Msimbazi Simba sc kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Mechi hii ya kulinda heshima kwa timu zote ilianza kwa timu zote kucheza kwa umakini, lakini Simba walionekana kutawala mchezo huo na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa Yanga.

Katika kipindi hicho cha kwanza, Amiss Tambwe, Said Ndemla kwa nyakati tofauti walipata nafasi nzuri za kufunga lakini kukosa umakini kuliwanyima Simba mabao.

Yanga nao walifika mara kadhaa langoni mwa Simba, lakini Mrisho Ngassa na Didier Kavumbagu walishindwa kuzibadili nafasi hizo kuwa mabao.

Kwa ujumla kipindi cha kwanza kilikuwa katika himaya ya Simba kwasababu walifika mara nyingi zaidi langoni mwa Yanga na pengine katika mechi za nyuma wangekuwa wanacheza mpira kama ule wasingekuwa hapo walipo.

Kipindi cha kwanza kilimazika kwa timu hizo kutofungana.

Kipindi cha pili, Yanga walitawala zaidi mchezo, lakini dakika 75 Haruna Chanongo aliifungia Simba bao la kuongoza.

Dakika ya 86 ya kipindi hicho, Saimon Msuva alichomoa bao hilo na mechi kumalizika kwa sare ya 1-1.

Hata hivyo katika mchezo huo kulitokea vituko kadhaa.

Cha kwanza ni mshambuliaji wa Yanga Didier Kavumbagu kutoa taulo la mlinda mlango wa Simba Ivo Mapunda alilolitundika kwenye nyavu golini.

Kitendo hicho kinatafsiriwa kuwa ni imani za kishirikina kwa wachezaji wa Yanga walioamii taulo hilo limezuia mabao.

Kutokana na purukushani hiyo, mwamuzi wa mchezo huo alimzawadia kadi ya njano Kavumbagu na Ivo akapewa taulo lingine.

Dakika chache baadaye, shabiki mmoja aliingia uwanjani na kuiba taulo la Ivo na kulirusha kwa mashabiki wa Yanga, lakini alitiwa mbaroni na Polisi walioshindwa kumuona wakati anaingia.

Hata hivyo baada ya Simba kufunga bao, dakika chache baadaye, kocha msaidizi wa Simba, Suleiman Matola na kocha wa makipa Idd Pazzi walitolewa ka kadi nyekundu.

Kwa matokeo ya mechi zote endelea kutufuatilia na muda si mrefu utapata pamoja na uchambuzi.

No comments: