Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

YASEMAKEANA LULU AMEANZA KURUDIA MAMBO YA MCHARUKO YALIO MPOTEZEA DIRA KABLA



KWAKO Elizabeth Michael ‘Lulu’. Leo nimeona nikukumbuke kupitia barua! Natambua uwezo wako mkubwa katika kazi, juhudi zako binafsi ndiyo zimekufikisha hapo ulipo, mataifa mbalimbali sasa wanatambua kuwa kuna mtu anaitwa Lulu, yupo Bongo, muigizaji!.

Sitaki kukurudisha sana nyuma lakini najua unajua kuwa ni jinsi gani kipindi cha nyuma ulikuwa ukipamba vyombo vya habari kwa skendo chafu. Ulipoteza dira ya kimaisha, watu wengi waliokuwa wakikufuatilia kazi zako walianza kukutupa.


Walikupotezea kwa sababu ya matukio ya ulevi, mavazi ya nusu utupu na matukio mengi ya ajabuajabu yaliyofanana na hayo. Sina nia mbaya kukumbusha lakini waswahili wanasema binadamu anajifunza kutokana na makosa. Maishani mwako umekutana na mazito yasiyofanana na umri wako.
Kwenye ulimwengu wa mahaba, ilikuwepo minong’ono mingi juu ya watu wanaotajwa kushiriki mapenzi na wewe, walitajwa vigogo, mastaa na hata wasio mastaa. Sitaki kusema ni kweli au la lakini lisemwalo kama halipo, ujue laja.
Siri ilifichuka kupitia kifo cha yule unayedai alikuwa mwandani wako, marehemu Steven Kanumba.
Mazingira ya kifo chake, umri mdogo uliokuwa nao ilikuwa ni fundisho kubwa maishani mwako. Ulipambana na msalaba wa gereza, ukapambana na mlolongo wa kesi mahakamani hadi pale ulipofanikiwa kutoka kwa dhamana, Januari mwaka jana.

Baada ya kutoka mahabusu, kwa kipindi cha takriban mwaka mmoja sasa ulikuwa kimya, ulionekana kubadilika kitabia. Yale uliyokuwa ukiyafanya awali, uliyaweka pembeni na zaidi kusimamia mustakabali mzima wa maisha yako, ulikuwa mwema sana aisee!. Kinachonisikitisha ni kuanza kusikia tena matukio ya ajabu, unaonekana kubadilika. Nimefuatilia tabia zako, naona umeanza kubadilika, umesahau eeeh! Mavazi yako kwa miezi michache iliyopita, nimegundua yanaanza kuchepuka! Mfano mzuri ni kigauni ulichokivaa mwishoni mwa wiki iliyopita katika sherehe yako ya kuzaliwa. Hakikustiri maungo yako nyeti, kilionesha sehemu kubwa ya matiti yako.
Kama hiyo haitoshi, kupitia mitandao ya kijamii umeanza kushusha matusi mazito bila sababu za msingi, mtu akikukosoa kidogo, unampa maneno machafu ambayo hayaandikiki gazetini. Kama kioo cha jamii, unapaswa kuvumilia mengi. Nikiwa kwenye kazi zangu za kila siku, huwa nakuwa wa kwanza kupata fununu za mabadiliko ya kila msanii na namna anavyoishi. Nikuonye tu, kuwa makini na mwenendo wako kwani tayari jamii ilishaanza kujenga imani na wewe. Uliaminika na ndiyo maana ukapata bahati ya kuchukuliwa katika kampuni nzuri ikakusimamia kazi zako hadi sasa. Kwa kuwa tayari nimeanza kupata malalamiko kutoka katika vyanzo vyangu, nikusihi sana mdogo wangu, usirudi ulipotoka. Jenga heshima mpya na jamii ikuamini kutokana na kazi zako na si skendo za ajabuajabu, kwa leo ni hayo tu!
Wasalam.
Ni mimi Anko Erick Evarist. 
-GPL

2 comments:

Anonymous said...

Na wewe sijui uncle wake kama unampenda si umtafute umweleze hayo huko huko nyumbani kwenu? Unavyomwandikia barua na kuitanganza hivi ndio nini? Je unamwonea huruma au unamwonea wivu?

Huyo sio mtoto mdogo japo waliweza kusema alikua na miaka sijui chini ya 18 lakini uimwona utajua sio mdogo wa kiumri kama inavyodaiwa ila Tanzania unaweza kukata hata miaka 5 nyuma na watu walivyo wafupi wa kumbukumbu hata wasikumbuke. Ni mtu mzima na anajua nachofanya.

Na hiyo unavyomwita sijui star wakimataifa labda ni taifa la Kenya na Nigeria..Mimi mtanzania nina collection ya movies za Tanzania nyingi sana tu lakini huyu msichana nilikua simfahamu mpaka alovyomuua Kanumba. Sasa mkimpa kichwa kuwa yeye ni star wa kimataifa ndio mnamwengezea kichwa wakati hajulikani hata na watanzania wengine wanaoishi nchi za nje.

Hivyo mwache aishi maisha yake akiharibikiwa ni yeye, wewe kama unlce wake wa kweli mwite huko nyumbani umwambie hayo. Kupost hizi barua ndio zinaongeza watu kufikiria hivyo na huwezi jua mwenzako anafanya hivyo kwa nia gani "SEX SELLS" labda ni ili kujitangaza. Labda anajua wateja wake wanampenda akiwa malaya malaya.

kama unapenda mtafutie kazi aondoke kwenye hiyo fan till then mwache aishi atakavyo. ndio inamwezesha kuishi jiji la Dar Es Salaam.

Jay said...

Dogo bado hajakuwa....bao anadanganyika kitoto na madushelele ya mjini....asipo angalia atalostika kama Masogange anafikia kuchezewa tu kila kukicha huku midume ikimsanifu.