Kanali Dr. Edward Massala kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) akifuatilia majumuisho ya Mkutano wa Tatu wa Maadalizi ( Prep CoM) ya mapitio ya Mkataba wa Kimataifa wa Uzuiaji wa Usambaaji Holela wa Silaya za Nyukilia ( NPT) Mkutano huo wa maandalizi ulifanyikak wa wiki mbili hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Ingawa wajumbe kutoka nchi 149 kati ya 189 ambazo ni wanachama wa NPT hawakutoka na makubaliano ya pamoja kuhusu mapendekezo na mpango wa utekelezaji vinavyokusudiwa kuwasilishwa kwenye mkutano huo wamapitio utakaofanyika mwaka 2015. jambo la msingi ambalo kila nchi inalikubali ni kwamba hakuna nchi au shirika litakaloweza kukabiliana na madhara ya mlipuko wa silaha za nyukilia na kwamba jambo la muhimu ni kuondokana kabisa na silaha hizo ili dunia iwe mahali salama. Nyuma ya Kanali Massalla ni Bw. Abdalla Khamis, Afisa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Mkutano wa Tatu wa maandalizi ( Prep Com) ya
mkutano utakaofanyia mapitio ya
Mkataba wa Kimataifa Unaozuia Usambaaji Holela wa Silaha za Nyukilia ( NPT) umemalizika mwishoni
mwa wiki iliyopita, huku wanachama wakitoka bila ya kuwa na makubaliano ya pamoja kuhusu
mapendekezo na mpango wa utelelezaji yatakayowasilishwa
katika mkutano huo wa mapitio
unaotarajiwa kufanyika mwaka
2015.
Licha ya kwamba nchi
hizo hazikutoka na makubaliano ya
pamoja, jambo la msingi na ambalo
linakubalika na wote ni kwamba
hakuna nchi au shirika la kimataifa linatakaloweza kukabiliana na madhara
ya mlipuko wa silaha za nyukilia iwe kwa
makusudi au kwa bahati mbaya.
Na kwa sababu hiyo nchi
136 zilizochangia hoja ya madhara
ya silaha za nyukilia kwa binadamu zilisisitiza kuwa njia pekee ya kumwepusha mwanadamu na madhara hayo ni kuondokana au kuachana kabisa na silaha za hizo.
Hata hivyo, nchi zinazomiliki silaha za nyukilia ambazo
ni Ufaransa, Marekani, Uingereza, China na Urusi, licha ya
kutambua madhara ya silaha hizo, zenyewe
zimependekeza kuwa upunguzaji wa silaha
hizo, ufanyike hatua kwa hatua.
Akizungumza na
waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano
huo uliofanyika kwa wiki mbili
kuanzia April 28 hadi Mei Tisa,
Mwenyekiti wa mkutano huo wa Tatu
Mwakilishi wa Kudumu wa Peru katika Umoja wa Mataifa, Balozi Enrique Roman – Morey alieleza kwamba kutofikiwa kwa makubaliano ya pamoja kuhusu
mapendekezo na mpango wa utekelezaji hakukutokana na kutokuwepo wa utashi wa kisiasa baina ya wajumbe bali ni ufinyu wa muda
zaidi wa majadiliano.
Kwa mujibu wa Balozi
Morey nchi 149 kati ya 189 ambazo ni wanachama wa NPT
walihudhuria mkutano huo. Na kwamba nchi tano zinazomiliki silaha za nyukilia
yaani Marekani, Urusi,
Uchina, Ufaransa na Marekani, ziliwasilisha taariza zao zinazofanana
kuhusu mchakato unaoendelea wa kupunguza
malimbikizo ya silaha hizo.
Mwenye kiti huyo
wa Prep Com alibainsha kwamba nchi wa
wanachama wa NPT walijadili vipengele
muhimu vinayounda NPT ambavyo ni uzuiaji wa usambaaji holela wa silaha za
nyukilia, upokonyaji wa silaha za
nyukilia, matumizi salama ya nishati ya nyukilia, madhara ya
nyukilia kwa mwanadamu na Uanzishwaji
wa Ukanda huru dhidi ya silaha za
nyukilia na silaha zingine za maangamizi katika eneo la Mashariki ya kati.
Aidha
Balozi alieleza pia kwamba jambo jingine lililojadiliwa kwa mapana na
wanachama wa NPT ni kuhusu haja na
umuhimu wa mataifa kuridhia mkataba wa
kimataifa unaozuia majaribio ya silaha za nyukilia (CTBT). Hadi sasa ni nchi 162 tu ndizo zilizoridhia mkataba huo.
Jambo la muhimu ambalo Mwenyekiti wa PrepCom anasema lilionekana dhahiri katika mkutano huo ni kuwa nchi zote zilizoshirikia mkutano huo wa maandalizi, zimeonyesha uwajibikaji katika kuhakikisha kuwa Dunia inaondoka na inakuwa huru dhidi ya silaha za
nyukilia.
Mapendekezo na mpango
wa utekelezaji uliopitishwa mwishoni mwa mkutano huo, utawasilishwa na Mwenyekiti wakati wa mkutano wa mapitio ya NPT
utakofanyika mwezi Mei mwaka 2015.
Ujumbe wa Tanzania
katika mkutao huo uliongozwa na Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika
Umoja wa mataifa, Balozi Ramadhan Mwinyi
akiwamo mtaalamu
kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania,
Kanali Dr. Edward Massala.
No comments:
Post a Comment