
Mhubiri wa ‘kanisa la kupapasa’ anayejiita nabii Tito Mwanzalima mara kadhaa anaingia ndani ya daladala kuanzia Kimara hadi Mbezi jijini akiwashauri watu kunywa pombe, kuzaa na wafanyakazi wa ndani na kuoa wanawake wengi kwani ndicho Mungu wake anayemuamini alichoagiza.
Mwanzalima ambaye anavaa mavazi yasiyo nadhifu , rozari na kofia akiwa pia amefuga ndevu nyingi huwaambia abiria kuwa pombe ni dawa ya tumbo na maradhi mengine hivyo wanywe kwa kuwa imeandikwa kutumia kilevi kwa afya.
Akinukuu vifungu vya Biblia kutoka Waraka wa Paulo kwa Tito. kitabu cha Mithali na Mwanzo alisema pombe inaruhusiwa pia wanaume wana haki za kuzaa na watumishi wa ndani na pia akishauri kuwa na wanawake wengi.
Wakati anahubiri alihojiwa na baadhi ya abiria waliotaka kujua iwapo mafundisho ya kanisa lake yanaruhusu wanawake kuzaa na watumishi wa kiume lakini alipinga na kutakiwa kueleza sababu lakini hakuwa na maelezo.
Tito alidai kuwa kanisa lake linafanyakazi Kigamboni na alipoulizwa iwapo limesajiliwa hakuwa na jibu.
Aidha nabii huyo muda wote anahubiri kuhimizia kutenda mambo yanayokatazwa na maandiko matakatifu. Hata hivyo mahubiri yake hayakubiliki kwa abiria anaowapa ujumbe na wengi wanakataa kununua vitabu wakimuona kama aliyechanganyikiwa.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment