ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, May 31, 2014

KINANA ATAKA MIGOGORO YA ARDHI KITETO ITAFUTIWE UFUMBUZI WA KUDUMU SASA NA SI BAADAE


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wakazi wa Kiteto mjini kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya na kuwaambia kuwa wilaya hito imekuwa na matatizo makubwa ya ardhi ambayo inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa kudumu sasa na si baadaye.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa vyama vingi vya siasa vimekuwa kama wasanii wa kuigiza havina sera na vimekuwa vikiishi kutokana na matukio.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa Kibaya wilayani Kiteto wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kwenye uwanja wa mpira wa Kibaya.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akichagua Tshirt ya Chama kutoka kwa wakina Mama Wajasiriamali wanaouza nguo za CCM wilayani Kiteto.
Nguo za CCM zimekuwa zinauzwa katika kila kona nchini na kuvaliwa na watu wengi ambapo inakadiriwa CCM ina wanachama zaidi ya milioni sita nchi nzima na idadi imekuwa ikiongezeka siku hadi siku.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Wazee wa Kimasai katika kijiji cha Kimotoro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wanakijiji cha Irkiushbor wakati wa mapokezi mpakani mwa wilaya ya Simanjiro na Kiteto.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiruka juu kama Morani wa Kimasai alipotembelea kjiji cha Partimbo Eseki na kukagua miradi ya maji.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda mti wa kumbukumbu alipotembelea shule ya msingi ya Laalakir .Shule hiyo ya msingi ni ya jamii ya wafugaji ambayo inafanya vizuri katika wilaya ya Kiteto.
Wanakijiji cha Kimotoro wilayani Simanjiro wakizungumza na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na kumuomba awasaidie kumaliza migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na hifadhi.

1 comment:

Anonymous said...

Ndg yangu Nape, yaani huna la zaidi ya kuwazungumzia wapinzani kwani wao sio wanasiasa. Hebu jaribu kutueleza maswala muhimu ya kuendeleza taifa la tanzania, inaelekea hujui siasa kabisa kwani una ubaya na wanasiasa wengineo, tueleze umefanya nini na utafanya nini hapo baadae sio ubaya!! Tunachoka kusikia hilo hilo kila leo!!