ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 27, 2014

KINANA:PUNGUZENI SIASA HANANG


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katesh wilayani Hanang ambapo aliwaambia wananchi wanapaswa kushirikiana na serikali yao katika kuleta maendeleo na kuachana na mambo mengi yanayoendelea kwenye siasa.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katesh kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo ambapo aliwaambia wananchi CCM imejipanga vizuri sana kiasi cha wananchi wengi kuendelea kuiamini ,alisisitiza nchi nzima ofisi za CCM zinajengwa na wanachama wake wakati wapinzani ofisi zao ni za mifukoni.

Mbunge wa Jimbo la Hanang Mama Mary Nagu akihutubia wananchi wa Katesh ambapo pamoja na kueleza mipango ya maendeleo pia alitoa mizinga ya nyuki kwa vikundi vya ujasiriamali.

Mabinti wa Kibarbeig wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Katesh.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Endasak ambao aliwaambia migogoro mingi waliokuwa nayo ni kwa sababu ya kuhusisha kila jambo na siasa,miradi inakataliwa kwa sababu za kisiasa hivyo waweke siasa pembeni wafanye maendeleo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga mpira kuashiria kuzinduliwa kwa  mashindano ya mpira wa miguu ya CCM Cup Endasak, Golikipa aliyekuwa golini wakati mpira unapigwa ni Mbunge wa Jimbo la Hanang Mama Mary Nagu.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Mbunge wa Jimbo la Hanang Mary Nagu,Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye na Mkuu wa Wilaya ya Hanang Christina Mndeme wakishiriki pamoja na wananchi ujenzi wa ofisi ya CCM Tawi la Qaloda.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Basoutu na kuwaambia wachague Viongozi wa kijiji watakaosaidia kuleta maendeleo na si viongozi watakaorudisha nyuma maendeleo na kuwasababishia migongano mikubwa kama ya ardhi inayoendelea sasa.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye baada ya kumaliza mkutano na wanakijiji ambao wanamgogoro wa ardhi wilayani Hanang.

Kinana na Nape wakimhoji vizuri Mwenyekiti wa Chadema wa Wilaya ya Hanang, Augustino Mayumba aeleze alikopeleka hati ya mkataba wa mnara wa simu wa Vodacom uliowekwa katika Kijiji cha Basouto ambao alishiriki kutia saini ambapo hadi sasa malipo ya fedha za mnara huo  haijulikani nani analipwa.
Hatua hiyo ya kumhoji ilitokea baada Kiongozi huyo kuuliza swali kwenye mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Kijiji cha Basouto kuwa viongozi wa CCM wanakula fedha za malipo ya mnara huo uliowekwa eneo la soko. Kinana alimtaka Mayumba aeleze mkataba huo ameuweka wapi. Licha ya kiongozi huyo wa Chadema kukiri kushiriki kusaini mkataba huo lakini alishindwa kueleza kwa kusema kuwa na yeye hajui mkataba huo ulipo, jambo ambalo liliwafanya wananchi kuanza kumzomea. Kinana aliwataka wananchi na serikali kumbana Mayumba hadi aeleze alipouweka mkataba iliserikali ya Kijiji iwe inapata malipo hayo.(Picha kwa Hisani ya Bashir Nkoromo).

No comments: