| Solomon Mukubwa akiwa katika pozi na mtangazaji wa Wapo Radio Fm Silas Mbise. |
Mukubwa amesema mama huyo alimrushia mapepo yaliyosababisha mkono wake kuanza kuoza kila iitwapo leo hadi kufikia hatua ya kuambiwa hospitalini kwamba inatakiwa mkono huo kukatwa kama anahitaji kuendelea kuishi hali iliyolazimu akubaliane na uamuzi huo wa madaktari hivyo mkono wake mmoja kukatwa baadaye Solomon aliokoka na kumjua Mungu hivyo kujikita katika imani yake ya kumwamini Mungu ambapo mama yake huyo naye alipata kilema cha macho ( kama nakumbuka vyema) Pia mama yake huyo alikiri kuwa ndiye aliyehusika na ulemavu huo wa mkono wa Solomon.
Hata hivyo pamoja na hayo yote Solomon Mukubwa alimsamehe mama yake huyo pia huwa hapendi kuzungumzia kisa hicho zaidi anataka kumtangaza Kristo, kisa hiki ni kirefu na mengi nimeyaacha kama unayakumbuka endelea kwa kukomenti chini ya habari hii. Pia GK inatarajia kumtafuta Mukubwa ili ipate kisa kamili.
No comments:
Post a Comment