Advertisements

Saturday, May 24, 2014

LEO NDIO LEO NEW YORK NA DMV NANI KUTOKA KUFUA MBELE?, NEW YORK IMEISHATINGA DC ASUBUHI HII

New York Dream Team (NYATI)
Timu ya DMV

Wahenga walisema leo ndio leo asemaye kesho muongo na mkamia maji sana hushiindwa kuyanywa kama yale majigambo ya timu ya New York na DMV leo itafikia mwisho hapo zitakapako malizika dakika 90 za mchezo na kuamua nani atakaye ibuka mshindi wa mtanange huu unaosubiliwa kwa hamu sana na mashabiki wa pande zote mbili hususani DMV na vitongoji vyake.Zege halilali lazima kieleweke leo ni maneno ya NY Ebra na kulinganisha mechi ya leo ni sawa na sungura kumkaba kobe.

Mechi hii imekuwa gumzo na kuleta wasi wasi kwa wachezaji wa pande zote mbili kuhofia kufungwa baada ya matambiano ya muda mrefu kwenye mitandao ya kijamii ukiondoa kocha wa timu ya New York Salim Akida ambaye yeye amesema anatarajia ushindi leo DMV mechi itakayoaanza saa 10:30 jioni na wachezaji wa timu zote wametakiwa kufika uwanjani nusu saa kabla ya mchezo.

Wasiwasi mwingi unaonekana kuikumba DMV kwa sababu ya kutokua na damu changa nyingi kwenye timu yao kongwe na yenye uzoefu kwenye mechi kama hizi ambazo huibuka mshindi siku zote. Timu ya New York ambayo inatamba kwa utandazaji soka ya kisasa na yenye vijana wendao kasi na kujiita "NYATI" kwa maana ya kuwa wakali wanapokua uwanjani hasa wanapocheza mechi yenye upinzani kama huu.

Mechi ya leo imedhaminiwa na The People's Bank of Zanzibar (PBZ) ambao wamelipia uwanja, marefa, maji na mpira utakaochezewa na mgeni rasmi wa mpambano huu wa kihistoria ni Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula.

Makocha wa timu zaote mbili wameogopa kutaja vikosi vitakavyoanza na timu ya New York ipo vizuri na haina majeruhi. Timu ya DMV inamajeruhi wawili Yusuf ambaye aliumia kufundo cha mguu wa kushoto kwenye mechi ya Diaspora World Cup ambayo yeye alifunga goli moja kati ya matatu yaliyofungwa dhidi ya Senegal na Libe anayesumbuliwa na maumivu ya misuli. Mbali na wachezaji hao wengine wote katika timu ya DMV wapo na ari kubwa ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo itakayochezewa uwanja uliopo Walker Mills Park anuani ni 8001 Walker Mills Rd, Capitol Heights, MD.

3 comments:

Anonymous said...

PBZ ingesaidia zaidi wananchi wa Zanzibar ambao ndio wanaochangia benki hiyo. Wachezaji wa mpira wa DMV na NY hizo ni starehe zao na wanapaswa wajihudumie wenyewe badala ya kutumia jasho la wengine ambao hawanufaiki na hiyo mechi. Ingalikua mechi hiyo inachezewa eneo ambalo wananchi walio wengi wa Zanzibar wanaweza kupata fursa ya kuona mechi hiyo hapo ingekuwa sawa kudhamini mechi hiyo. Mimi nauliza kwa nini PBZ inatumia jasho la wananchi kwa kuhudumia shughuli ambazo wanaochangia benki hiyo hawanufaiki ipasavyo. Hizo gharama zitazotumika hapa zingetumika kwa maendeleo ya wananchi wa Zanzibar

Anonymous said...

Udhamini WA mechi unasaidia benki kujitangaza kwenye diaspora community ambayo let's face it, inatuma pesa nyumbani. Pesa hiyo inasaidia jamii. Ndugu wanaenda madukani, watoto wanaenda shule, Ndugu WA a we Kay pesa benki etc etc. Tusiwe tunapenda kulalamika Sana. inabidi tufikirie mambo kwa urefu na undani. Kibiashara
Great job Dj Luke Joe

Anonymous said...

NY Team continue dreaming! It shall come true!!