Mtanzania Ndugu Bruno aliyekaa Upande wa Kulia ndiye aliyeshindwa kujizuia na Kuamua kuaniaka hisia zake kuwa Mh:Mwigulu Nchemba ni "RISINGI STAR"
Ni nadra sana mtu Kusimama mbele ya Umma na Kuonesha hisia Zake kuhusu Kiongozi Flani namna anavyomkubali Kiutendaji na kufikia hatua ya Kusema anatamani Kuona Siku moja Nchi yake Inaongozwa na Kiongozi huyo.Lakini imetokea kwa Mtanzania huyu(Pichani) aliyeamua kunika hisia Zake kwa Watanzania waliokusanyika pamoja kwenye Ufunguzi wa Shina la CCM-Maryland Nchini Marekani namna anavyopendezwa na Utendaji kazi wa Mh:Mwigulu Nchemba,na kudiriki Kusema "Watamdharau,Watamdhihaki,Lakini ipo siku Watamkubali na Atawaongoza" akatolea Mfano kuhusu Rais wa Marekani Barack Obama alivyodhihakiwa hapo awali wakatia anajiandaa Kugombea Urais awamu ya Kwanza na yapili,lakini hii leo Obama ni nani kwa Marekani?Hivyo anasisitiza Kunahaja kwa Watanzania Kumuunga Mkono Mwigulu Nchemba katika siasa Zake kwa sababu zimejikita kutetea Watanzania,Kuimarisha Uzalendo na Kupigania Umoja na Mshikamano ndani ya Taifa letu.Angalia Video hii hapa Chini ya Mtanzania huyu (Bruno)akitoa hisia zake kwa Mh:Mwigulu nchemba.
Angalia Vidoe hii hapa.
5 comments:
Njaa mbayaaaa...Looooooohh!!!!
-PAKAJEUSI
Huyu mbeba box anatafuta ukuu wa wilaya. mambo ya DMV yamemwia magumu!!
hivi kwanini watanzania hampendi kuwa wa kweli sasa hapa mnaumia nini kisa ameamuwa kuwa mkweli ??Huwo ndiyo mtazamo wake sasa wewe unapata hasira za nini ?? kwani mpiga mabox hana hoja?? tueshimu mawazo ya watu watanzania ...Laaah sivyo atutaendelea
Wabongo kwa njaa bwana...Sasa wewe Bruno mtu mzima unaajiadhirisha kwa hoja muflisi zisizo na mashiko...mbona unajishusha kwa kauli mbofu mbofu namna hii...
hawa wote ukiuliza kazi zao utachoka hahahahaaaaaa
Post a Comment