Na Andrew Chale
MBUNIFU na mwanamitindo (model) Rodrick Charles maarufu kwa jina la ‘Rodney de lativo’ amefariki dunia jana (Mei 30) baada ya kuugua kwa muda alipokuwa amelazwa Hospitali ya Jeshi, Lugalo.
Akizungumza na Mtandao huu mapema leo kwa njia ya simu, Rafiki wa karibu wa familia ya marehemu, David Msangi alisema marehemu alipatwa na umauti alipokuwa akiendelea na matibabu katika Hospitali ya Lugalo, alipokuwa amelazwa na msiba huo hupo nyumbani kwa marehemu Tabata Bonyokwa.
“Tumempoteza mtu muhimu sana ambaye alikuwa na mawazo mengi ya kufikia mafanikio yake. Tutaendelea kumkumbuka.” Alisema Msangi ambaye pia alikuwa mshahuri wa karibu wa marehemu.
Msangi alisema kwa mujibu wa familia ya marehemu, anatarajiwa kuzikwa hiyo Jumamosi Mei 31huko huko kwenye makaburi ya Tabata Segerea.
Wakati wa uhai wake, marehemu alifanya kazi kwenye majukwaa mbalimbali na wabunifu na wanamitindo wakubwa wakiwemo wabunifu Ally Remtullah, Mustapha Hassanali, Asia Idarous. Wanamitindo Rio Poul, Martin Kadinda, Justine, Faustine Simon na wengine wengi.
Rodney mpaka anakutwa na umauti, alikuwa mshahuri na model wa kampuni ya Crisswelly African Fashion.
Mareehemu alizaliwa Mei 26, 1994. Elimu yake alisomea Magoze Sekondari na kuhitimu 2011 na kuingia moja kwa moja kwenye fani ya uwanamitindo na kuendelea hadi alipokutwa na umauti.
Aidha, kwa jamaa wa karibu na wabunifu na wanamitindo kwa watakaotaka maelezo ya kufika kwa marehemu wanaweza kuwasiliana na David Msangi kwa namba hii 0652901684
..Rest In Peace Rodney. I remember you forever.
No comments:
Post a Comment