Baadhi ya Viongozi Wakuu wa
Afrika waliohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika
ambao ulifunguliwa na Mh.Rais wa Rwanda Paul Kagame. Mh.Kagame katika hotuba yake
alisisitiza kuzijengea uwezo sekta binafsi ili Afrika iweze kufikia uchumi wa
kati kwa kipindi cha Miaka 50 ijayo. Aidha katika kufikia lengo hilo Rais
Kagame alisema hatuna budi Afrika kuachana na Migogoro na kutekeleza kwa
vitendo makubaliano yanayoafikiwa na Viongozi wa Afrika ili kujenga uchumi imara kwa vizazi vijavyo.
Kikundi cha Ngoma za asili cha
Bollet Nationol – URUKEREREZA cha jijini Rwanda kikitumbuiza wakati wa ufunguzi
wa Mkutano Mkuu wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika unaofanyika Rwanda.
Mh.Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum na Washiriki mbalimbali
wa Mkutano wa mwaka wa Benki ya Maendeleo ya Afrika mara baada ya ufunguzi wa
Mkutano huo uliofunguliwa na Mh.Paul Kagame katika ukumbi wa Mount Karisimbi
Jijini Kigali Rwanda.
.jpg)

.jpg)
No comments:
Post a Comment