Wednesday, May 21, 2014

MASAHIHISHO YA MAJINA YA WANACHAMA HAI KWENYE TANGAZO MAALUM

UCHAGUZI WA VIONGOZI JUMUIYA YA WATANZANIA DMV
Kamati maalum ya uchaguzi DMV inapenda kuwakumbusha wanajumuiya kuhusu taratibu za uchaguzi. Uchaguzi utafanyika kufuata katiba iliyotungwa na wanajumuiya wenyewe. Rejea sehemu zifuatazo za katiba yetu: 1.2 Haki za wanachama (Rights of Members) na 1.3 Wajibu wa wanachama (Obligations of Members). Katiba ya Jumuiya ya Watanzania (DMV) inapatikana hapa: http://www.watanzaniadmv.org/about.asp.
Orodha ya majina ya wanachama hai inapatikana hapo chini. Tunawaomba wanajumuiya muangalie majina yenu na mjiunge na jumuiya yetu ili tuweze kupiga kura na kuchagua viongozi wetu. Lengo letu ni kujenga Jumuiya iliyo imara na hakuna atakayeweza kufanya hivyo kwa ajili yetu bali ni sisi wenyewe. Katiba tuliiweka ili ituongoze huu ni wakati muafaka wa kurekebisha makosa na kuanza upya bila kuvunja sheria za katiba yetu.
Wasiliana na muweka hazina wa Jumuiya kuhusu suala lolote la malipo: Ndugu Genes Malasy kupitia barua pepe gmalasy@watanzaniadmv.org au kwa simu nambari (301) 367-8151.

Kwa maswali au mawazo wasiliana na kamati ya uchaguzi kutumia barua pepe ifuatayo; uchaguzi2014@gmail.com

Tunatanguliza shukrani,
                          Kamati maalum ya Uchaguzi




“UMOJA NI NGUVU NA UTENGANO NI UDHAIFU”

WANACHAMA HAI
1    Amos    Cherehani
2    Asha    Hariz
3    Asha    Nyang'anyi
4    Benson    Mwaipaja
5    Cane    Mwihava
6    Dickson     Mkama
7    Dj Luke   
8    Eliserena    Kimolo
9    Elizabeth    Kibona
10    Ernest    Kessy
11    Farida    Jettah
12    Genes     Malasy
13    Grace     Mgaza
14    Hamza    Mwamoyo
15    Harrieta    Shangari
16    Iddy    Sandaly
17    Jabiri    Jongo
18    Jasmine     Rubana
19    Liberata    Mulamula
20    Martha    Lema
21    Mussa    Shedafa
22    Raymond    Abrahamu
23    Safari    O'Humay
24    Shamis     Mattar
25    Jacob    Kinyemi
26    Baraka     Daudi

8 comments:

Anonymous said...

Watu elfu tatu wakowapi? Hii ni aibu!!Mbona sikukumbushwa?! mama weeee!!!

Anonymous said...

Haya muda ndoo huu haya mnakumbushwa tena bado muda upo.

Anonymous said...

HATA MAAFISA WETU WA UBALOZI WAKO NYUMA PIA?

Anonymous said...

Habari ndiyo hiyo angalau balozi wetu kaonyesha mfano bora sasa maofisa wake jeeee?? Miaka ya nyuma balozi ndiyo alikuwa mlezi wa Jumuiya kwa maana hiyo maofisa wake nao walikuwa wana jumuiya...
Tutafika tuu.
Wajasiriamali mngejiandikisha ili muongeze wateja, muwe na bei za members na non-members. Ni ushauri tuu

Anonymous said...

Kwa haraka haraka, zaidi ya 50% ya wanachama hai wa Jumuiya ni viongozi watendaji na wajumbe wa bodi pamoja na familia zao. Hapa ndipo viongozi wetu inabidi waoneshe leadership skills zao. Leadership is not about photo op-ed, which appears to consume the mind of our novice leaders. Picha zenu na mawaziri na watu wengine mashuhuri won't move this Community forward, but effective leadership will!

Anonymous said...

Anonymous wa MAY 22 3.05PM wacha majungu, viongozi hawa wamejitahidi sana kufanya kazi na hujui wamekupigania kiasi gani wakati wa kikutana na hao viongozi wa nchi. Wametuletea mambo ya maendeleo na kutuconnect na nyumbani na mashirika makubwa yanayotoa huduma za jamii kama NSSF na mabenki na tukawaeleza madukuduku yetu leo hii benki hizi zimefungua account maalum za wanadiaspora.. Mikutano hiyo hiyo na viongozi wa serikali wamewaeleza kilio chetu kuhusu dual citizenship. VIONGOZI MTAKAORUDI ili muwakate vilimilimi wasiopenda maendeleo NAOMBA KILA MKITUTANA NA VIONGOZI WA SERIKALI NAOMBA ILE HOTUBA RAIS WETU UNAYOTOAGA NAOMBA UWAELEZE WANAJUMUIYA YAKO YALE ULIYOONGEA NA WAHASHEMIWA. ILI WAONE MNAVYOCHAPA KAZI. THESE GUYS HAVE DONE WONDERS FROM A BROKEN COMMUNITY NA SASA Tunaumoja wenye nguvu, tumepata misiba hapa last year kama vile kulikuwa na balaa these leaders stood with us na hajawahi chomwa mtu. LET US GIVE THEM POSITIVE CRIRICISM ILI WANAOKUJA WAENDELEE NA SI KUKAA HUJUI KINACHOFANYIKA UNAKAA KUANDIKA HABARI ZA UONGO. MPIGIE RAIS WAKO MWULIZE RAIS NILIKUONA UMEPIGA PICHA NA RAIS KIKWETE ALIPOKUJA LAST TIME HIVI MLIONGEA NINI??? AKISEMA NOTHING THEN COME AND WRITE YOUR IDEAS<<<,
TUWE WAKWELI

Anonymous said...

Nyie mnaodai mna leadership skills njooni! UTAMU AU UCHUNGU WA NGOMA UTAIJUA NA WEWE UKIINGIA NA KUICHEZA SI KWA KUKAA NA UNALALAMIKA OOOH MBONA VIUON VIMEKAZA?? INGIA UJARIBU NA WEWE KUZUNGUSHA KIUNO

Anonymous said...

Namuunga mkono mchangiaji anayekosoa uongozi. Wale wanaojua hawawezi kuongoza hawagombei nafasi za uongozi. Ukigombea ukachaguliwa ni lazima uongoze kwa ufanisi. Ni aibu kubwa kwa Jumuiya yenye watu zaidi ya 500 kuwa na wanachama hai wasiozidi asilimia tano. Kama kiongozi lazima ujiulize maswali mengi. Kuongoza ni kuhamasisha wafuasi kufanya kitu fulani kwa manufaa yao. Kiongozi asiyeweza kuhamasisha hawezi kuongoza kwa tija. Huu ni ukweli usiopindika.