Meneja wa kituo cha Sengerema FM Redio, Ndg. Felician Ncheye, akitoa nasaha za ukaribisho kwa washiriki wa mradi wa SHUGA na mgeni rasmi. Katikati ni Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu na Kulia ni Afisa Mipango VVU/UKIMWI UNESCO, Ndg. Herman Mathias.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, SENGEREMA - MWANZA
Redio za jamii nchini zimeaswa kutumika vizuri katika kuelimisha kamii juu ya kupambana na maambukizi ya virusi vya UKIMWI kupitia vipindi vya redio.
Hamasa hiyo imetolewa na Ndg Geofrey Mabu ambaye ni mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS wakati akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya ujulikanao kama SHUGA, unaotekelezwa na shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana Shirika la Mfuko wa Watoto (UNICEF) inayofanyika katika kituo cha Redio Jamii Sengerema mkoani Mwanza.
Mabu amesema kuwa mradi huo umekuja wakati muafaka ambapo malengo yake yakizingatiwa na kutekelezwa kama ilivyopangwa utasaidia kufikia malengo ya serikali ya kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI hadi Zero.
Mgeni rasmi Mratibu wa UKIMWI halmashauri ya Sengerema mkoa wa Mwanza kupitia mradi wa TACAIDS, Ndg. Geofrey Mabu akifungua warsha ya siku tatu ya mradi mpya kuhamasisha Vijana kuhusu udhibiti wa Maambukizi mapya ya VVU ujulikanao kama SHUGA.