Katika maisha, mara nyingi mambo mengi haswa yale ya maendeleo
unapoanza kufanya unakutana na vishawishi na vikwazo vingi, watu wengi
hukata tamaa pale wanaposhindwa kukabiliana na vishawishi hivyo, haswa
pale katika ndoto za
mtu akijaribu kukamilisha jambo fulani afike mahali
anapotaka, hii imetokea kwa watu wengi sana, ila mmoja wapo ni huyu
msanii Davido kutoka nchini Nigeria,ambaye kwa hivi sasa jina lake siyo
lazima uingie google kumjua, kila mtu namfahamu fika kama King wa
Skelewu.
Davido mwenyewe aliwahi kukiri kuwa hatosahau alichowahi kufanyiwa na
Baba yake mzazi, kama walivyo wazazi wengi wa hapa Bongo, pale
wanapoona mtoto ananza kujihusisha na maswala ya muziki, Davido
yalimkuta hayo hayo, Baba yake alikuwa anampinga vikali katika
kujihusisha na maswala haya ya muziki, akiwa bado anatoka(underground)
inasemekana kuwa, baba yake alikuwa anachukizwa na mambo aliyokuwa
anayafanya na alikuwa hataki kabisa kusikia mambo ya kujihusisha na
muziki, huku Davido kwa kujiamini aliendelea kufwata ndoto zake mwenyewe
na kupita pingamizi hizo kutoka kwa baba yake mzazi.
Hivi sasa Davido ni msanii mkubwa sana maarufu anayemiliki majumba na
magari ya kifahari kupitia muziki huo huo, na kwa jinsi inavyoonekana,
walishayasamehe yeye pamoja na baba yake mzazi nakuyaacha yapite, sababu
ameonekana mara nyingi akiwa na baba yake katika picha, ingawa baba
yake ni mtu tajiri sana, ila umaarufu wa Davido haukutegemmea hela za
baba yake, kutokana n kujiamini katika kipaji chake mwenyewe ambacho
ndicho kilichomletea mafanikio ambayo hadi leo Davido kujulikana karibia
Dunia nzima, haswa kwa hit single yake ya skelewu.
Vibe
No comments:
Post a Comment