Mwanamume mmoja wa Afrika Kusini
aliyewafungia wanawe kwa minyororo katika chumba kimoja kwa miaka
minane, amezuiliwa na polisi nchini humo.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 50,
alifikishwa mahakamani mjini Alexandra, mtaa ambao uko Kaskazini mwa
Johannesburg,kwa kosa la kutowalea wanawe vyema.miaka 14, 18 na 24, wote walikuwa na majeraha kwenye mikono yao na miguu.
Polisi wanasema kuwa watoto hao walipatikana baada ya mmoja wao mwenye umri wa miaka 24 ambaye pia ni mlemavu wa akili kutoroka.
Baba ya watoto hao alisema kuwa aliwafungia wanawe kwa usalama wao.
Polisi walikuwa na wakati mgumu kuwazuia wakazi waliojawa na gadhabu wakitaka kumshambulia mwanamume huyo na mkewe baada ya watoto wao kupatikana katika chumba hicho.
Majirani walitaja mazingira katika chumba hicho kama ya kusikitisha.
No comments:
Post a Comment