ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 3, 2014

BIA NA NYAMA CHOMA ISITUTOE ROHO JAMANI!



Mmh haya acha nikubali yaishe sipendi ubishi wa kijinga mie, eti kila kitu na wakati wake, nikibisha utasema najifanya najua kila kitu, lakini ukweli unabaki palepale vyote vina wakati lakini si mapenzi, mapenzi huongezwa shoga, si kupunguzwa, nani alikuambia katika mapishi kuna vitu hupunguzwa.

Sitaki kubishana sana na wewe unayejiita shangingi wa kisasa, kuna usasa katika mapenzi, mapenzi ukongwe shoga ndo maana ukimuona nyani mzee ujue kakwea minazi mingi na kukwepa mishale mingi.

Kama hujui uliza usijifanye kujua kumbe unaungua na jua, hakuna aliyezaliwa anayajua yote. Hata mimi nilikuwa siyajui, mengi nimejifunza kwa watu kwa kuambiwa kwa maneno au kukutana na watu wenye kujua shughuli yao.

Asikuambie mtu raha ya mapenzi umpate mtu mzima siyo vijana, wao nguvu nyingi kuliko akili. Lakini mtu mzima dawa utamsikia; “Binti haraka ya nini raha ya ngoma ufuate mdundo.”

Basi aaah, nawe unamfuata taratibu mnakata maji kama mamba, wazee hawana haraka, siyo wajinga waliosema ni zako zabibu basi kula taraaatiiibu kwa kujinafasi. Kila mmoja anafurahia safari siyo mtu akukomoe kwa vile umekula nyama choma na bia zake.

Basi anafanya mpaka ukienda msalani ujiulize jinsi ya kujisaidia au ukipata upenyo ukimbie na taulo la gesti.

Hayo siyo mapenzi bali kukomoana, kula vyako siyo sababu ya kutaka kuvilipa kwa njia ile, bali kukubali ni kupeana starehe yaani nipe nikupe na raha ya wimbo kupokezana au siyo mwakwetu?

Nia yangu haikuwa kuzungumzia haya kwa leo kwani hapo nyuma niliishagusia ila ni kukumbushana hasa ninyi wanaume mnaotoa ofa huku roho zinawauma, mwanamke kila anachoagiza unajisemea moyoni wee! kula lazima gharama utailipia kitandani.

Na mkishafika basi ndo kaaazi! Mpaka mwenzio chozi linamtoka, moyoni mwako kwa ulimbukeni unajiona wewe ndiye kidume, unajidanganya kidume si kumliza mwanamke kwa maumivu bali kumfikisha safari kwa raha. Jione kidume pale mwanamke anapotatalika kama bisi jikoni au kulia kilio cha raha na si cha maumivu.

Hivi kuna raha gani kufanya mapenzi na mwanamke mpaka apoteze fahamu, au akukimbie kwa vile umeamua tu kumkomoa. Tena nimesikia kuna baadhi ya wanaume hunywa pombe kali wapate kuchelewa kufika mwisho wa safari ili kumkomoa mwanamke.

Eeh jamani unanikomoa ili iweje, nimekulia nini kikubwa, yote kwa ajili ya vibia vyako na nyama choma na elfu tano ya Bajaj! Basi hao wanaohonga magari na nyumba wangekuwa hawanyanyuki kwa mwanamke mpaka waone amekata roho. Si ndiye aliyehonga pesa nyingi.

Ukahaba si dhambi ya kuhukumiwa kwa kufanyishwa mapenzi kama punda, kueni na huruma mnatuumiza sana, tutafanya nini lakini ugumu wa maisha isiwe kitanzi cha kutunyongea.
Japo tupo kwenye biashara lakini vilevile tunataka kuinjoi mapenzi si kukomolewa, usinywe pombe kali kunikomoa mwenzako. Sasa raha ya mapenzi ipo wapi kama unatumia nguvu nyingi starehe inakosekana, mwenzako najuta kukufahamu.

Na kibaya tukiachana unajisifu kwa wenzako kuwa ‘mkwaju’ mmoja ulichukua masaa mawili, jamani unafanya mapenzi na mtu au sanamu. Kwa kweli inaumiza inafikia hatua ya kutengeneza mtindo wa kuwakimbia wanaume kwa ajili ya ujinga wa watu wachache.

Ukiishamlia mtu vitu vyake, unajifanya unazungumza na simu kama humsikii vile na kuondoka eneo mlilokaa, lazima atajua unasikiliza simu ukifika sehemu ambayo hakuoni unatimua mbio.

Jamani nyama choma na bia zenu zisitutoe roho. Nafikiri ujumbe umewafikia walengwa, raha ya tamu utabasamu siyo mwenzio anasikia tamu wewe kama umelamba ndimu.
Kwa leo inatosha ni mimi anti Nasra Shangingi Mstaafu.

GPL

2 comments:

Anonymous said...

ahsante ahsante sana aunty nasra shangingi mstaafu kwa darasa hili muruwa lenye ukweli mtupu wanaume ndo walivyo wale wasionacho aliyenacho naha haja yakumkomoa mwanamke au kumnyiwa pombe kali.
ahsante sana aunty nasra wanawake someni hii story inaukweli mtupu

Anonymous said...

Post zako ni nzuri sa'aana