Jaiji Mfawidhi Mahakama Kuu kanda ya Iringa, Mary Shangali |
JAJI Mfawidhi wa
Mahakama Kuu Kanda ya Iringa, Mary Shangali amesema ipo haja kwa watu
wanaohukumiwa kwa makosa madogo kupewa adhabu mbadala ili kupunguza msongamano wa
wafungwa magerezani.
Aliyasema hayo
hivikaribuni alipofanya ziara yake ya kwanza wilayani Mufindi kwa lengo la
kufahamiana na watendaji wa mahakama hiyo na kukagua shughuli mbalimbali za
mahakama zinazofanywa wilayani humo.
“Zipo adhabu mbadala ambazo wafungwa wa kesi kama za wizi wa
kuku wanaweza kupewa badala ya kulundikwa magerezani katika mazingira haya
ambayo magareza zetu hazina uwezo wa kupokea wahalifu wengi,” alisema.
Alisema Mahakama ya
Tanzania ipo katika mabadiliko makubwa yenye nia na malengo ya kuhakikisha
kwamba kwa kushirikiana na wadau wengine wanamaliza changamoto mbalimbali za
kimahakama ikiwemo ya mlundikano wa mashauri ya zamani yanayozidi miaka
miwili mahakamani.
“Nia ni kutekeleza
azma yetu ya kutenda haki kwa wakati na kuwaondolea wananchi kero
zinazosababishwa na uchelewasheji wa haki,” alisema.
.
Katika ziara yake hiyo Jaji Shangali alikabidhi pikipiki nne
kwa mahakimu wa mahakama za mwanzo za Ifwagi na Kibao, Malangali, Kasanga na
Mgololo, zote za wilaya ya Mufindi.
Kutolewa kwa pikipiki
hizo, kumeelezwa na mahakimu wa mahakama hizo kwamba kutarahisisha utendaji
kazi wao na kuongeza ufanisi katika idara hiyo muhimu ya utoaji haki.
Katika ziara hiyo,
Shanghai alitembelea mahakamaa ya wilaya ya Mufindi na mahakama ya mwanzo
Mafinga, Sadani, Mlangali, na Iramba.
Katika taarifa yake
ya jumla ya mahakama ya wilaya hiyo, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mfawidhi,
Victoria Nongwa alisema mahakama hiyo inasimamia jumla ya mahakama 11 za mwanzo
zilizoko katika maeneo mbalimbali wilayani Mufindi.
Alizitaja mahakama
hizo kuwa ni Mahakama ya Mafinga mjini, Mufindi (Kibaoni), Kasanga (Igowole)
Malangali (Isimikinyi), Kibengu, Mapanda, Sadani (Utosi), Iramba (Itulavanu)
Mgololo, Ihanu (Ibwanzi) na Ifwagi.
Alisema mahakama hiyo
isiyo na mhasibu ina watumishi wa kada mbalimbali 31 ambao kati yao wanne ni
mahakimu wakazi wa mahakama ya wilaya na watatu ni mahakimu wakazi wa mahakama
za mwanzo.
Aliwataja watumishi
wengine kuwa ni mahakimu watatu wa mahakama za mwanzo wasio mahakimu wakazi,
mahafisa kumbukumbu watano ,wapiga chapa wawili, wahudumu wanne, walinzi nane
na dereva mmoja.
Katika kuboresha
utendaji wa mahakama hiyo, Nongwa ameomba msaada wa ujenzi wa mahakama ya
mwanzo Ifwagi na ukarabati wa nyumba ya hakimu wake.
Wakati mjini Mafinga
panatakiwa kujengwa upya mahakama yake ya mwanzo, alizitaja mahakama zingine
zinazohitaji ukarabati kuwa ni Mufindi (Kibao), Kasanga (Igowole) na Malangali
inayotakiwa kukarabatiwa choo na jengo la kutunzia vielezo.
Alisema mahakama hiyo
inahitaji pia kujengewa chumba cha mahabusu Malangali na fedha ya kuwezesha
kupatikana kwa umeme mbadala katika mahakama ya mwanzo Kibengu
Pamoja na maombi
hayo, wazee wa baraza la Mahakama ya Mwanzo Mafinga wameulalamikia uongozi wa
mahakama ya Wilaya hiyo kwa kutowalipa fedha zao za vikao vinavyohusisha kesi
zilizofutwa.
Akiwatia moyo kwa
kazi wanazofanya Jaji Shanghai alisema: “kuanzia sasa baraza la wazee litalipwa
fedha zao kwa wakati hata kama kesi wanazohudhuria zitahirishwa au kufutwa.
Akizungumzia utendaji
wa mahakama, Shaghai aliwaomba mahakimu kujiepusha na rushwa kwa
kuwa ni moja ya sababu inayokwamisha upatikanaji wa haki katika chombo hicho.
No comments:
Post a Comment