ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 12, 2014

IDADI YA WATALII HIFADHI YA RUAHA YAANZA KUONGEZEKA


Watalii ndani ya Hifadhi ya Ruaha

makundi ya tembo wa Ruaha

makundi ya Simba wa hifadhi ya Ruha
IDADI ya watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa imeanza kuongezeka ikiwa ni matokeo ya juhudi za uwekezaji na matangazo yanayofanywa na wadau mbalimbali katika kuitangaza hifadhi hiyo kubwa kuliko zote nchini.
Katika kipindi cha miaka minne iliyopota Afisa Utalii Mwandamizi wa hifadhi hiyo, Eva Pwele alisema kumekuwepo na wastani wa ongezeko la asilimia mbili ya watalii wa nje huku idadi ya wale wa ndani ikiwa ni ya kuridhisha.
Akizungumza timu ya wanahabari waliotembelea hifadhi hiyo hivikaribuni, Pwele alisema: “juhudi zinazoendelea kufanywa na serikali na TANAPA katika kuboresha miundombinu ya barabara za ndani na nje ya hifadhi zimnatarajia kuongeza watalii wanaotembelea hifadhi hii.
Alisema pamoja na juhudi hizo Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) inaendelea na mchakato wa kupata wawekezaji watakaongeza huduma za hoteli na uongozaji wa watalii ndani ya hifadhi.
Alisema wakati katika kipindi cha 2009/2010 watalii wa nje waliotembelea hifadhi hiyo walikuwa 11,040 wale wa ndani ambao wanasaidia sana kuamsha hali ya watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii walikuwa 8,039.
Kuanzia mwaka huo idadi yao iliongezeka na katika takwimu za 2010/2011, Pwele alisem wa nje walikuwa 12,885 na wa ndani 9,868 huku mwaka 2011/2012 wa nje wakiongezeka hadi 13,940 na wa ndani wakiwa 9,721.
Mhifadhi huyo alisema katika kipindi cha mwaka 2012/2013 watalii kutoka nje waliongezeka hadi 14,299 na wa ndani walifika 9,994.
“Ni matarajio yetu idadi ya watalii itaongezeka katika kipindi hiki cha 2013/2014; hiyo yote ni kutokana na mambo mengi yanayofanywa katika kuitangaza hifadhi hii yenye upekee,” alisema.
Alisema hifadhi ya Taifa ya Ruaha ipo katika eneo linalokutanisha ukanda wa kaskazini mashariki na kusini mashariki mwa Afrika na hivyo kuifanya iwe na aina mbalimbali za mimea na wanyama  ambao baadhi yake hawapo katika hifadhi nyingine.
Aliwataja naadhi ya wanyama wanaopatikana katika hifadhi hiyo kuwa ni pamoja na idadi kubwa ya tembo kuliko hifadhi nyingine yoyote Afrika Mshariki, aina 571 ya ndege wakiwemo wale wanaozunguka nchi mbalimbali, swala, tandala mdogo na mkubwa, samba, nyati, pundamilia, twiga, boko, mamba,  chui, mbwamwitu, nyani, mbwea na wengineo wengi.
Alisema katika hifadhi hiyo, wanafanya utali wa usiku ambao husaidia watalii kuona wanyama wasioonekana mchana, utalii wa kutembea kwa miguu ili kumfanya mtalii awe jirani na mazingira ya hifadhi na utalii wa masafa marefu kwa kutumia magari.
Ili kufika katika hifadhi hiyo, watalii wanaweza kutumia njia ya barabara kutoka mikoa mbalimbali kupitia Iringa Mjini au ndege kutoka viwanja vya Arusha, Songwe Mbeya, Dodoma, Dar es Salaam na Nduli Iringa

1 comment:

Anonymous said...

wanataka kuja kuwachukua wanyama hawa na kuwapeleka makwao wanaona nyinyi waafrica hamustahili kuwa nao hajui kuwatunza mnawatesa hawa wanyama bora wakakae katika ma zoo yao waingize pesa na watoto wao wawaone wanyama hawa mpoooo.kama hampo laleni usingizi