Watalii ndani ya Hifadhi ya Ruaha |
makundi ya tembo wa Ruaha |
makundi ya Simba wa hifadhi ya Ruha |
IDADI ya watalii wanaotembelea Hifadhi
ya Taifa imeanza kuongezeka ikiwa ni matokeo ya juhudi za uwekezaji na matangazo
yanayofanywa na wadau mbalimbali katika kuitangaza hifadhi hiyo kubwa kuliko
zote nchini.
Katika kipindi cha miaka minne
iliyopota Afisa Utalii Mwandamizi wa hifadhi hiyo, Eva Pwele alisema kumekuwepo
na wastani wa ongezeko la asilimia mbili ya watalii wa nje huku idadi ya wale
wa ndani ikiwa ni ya kuridhisha.
Akizungumza timu ya wanahabari
waliotembelea hifadhi hiyo hivikaribuni, Pwele alisema: “juhudi zinazoendelea
kufanywa na serikali na TANAPA katika kuboresha miundombinu ya barabara za
ndani na nje ya hifadhi zimnatarajia kuongeza watalii wanaotembelea hifadhi
hii.
Alisema pamoja na juhudi hizo Shirika
la Hifadhi za Taifa (TANAPA) inaendelea na mchakato wa kupata wawekezaji
watakaongeza huduma za hoteli na uongozaji wa watalii ndani ya hifadhi.
Alisema wakati katika kipindi cha 2009/2010
watalii wa nje waliotembelea hifadhi hiyo walikuwa 11,040 wale wa ndani ambao
wanasaidia sana kuamsha hali ya watanzania kutembelea vivutio mbalimbali vya
utalii walikuwa 8,039.
Kuanzia mwaka huo idadi yao iliongezeka
na katika takwimu za 2010/2011, Pwele alisem wa nje walikuwa 12,885 na wa ndani
9,868 huku mwaka 2011/2012 wa nje wakiongezeka hadi 13,940 na wa ndani wakiwa
9,721.
Mhifadhi huyo alisema katika kipindi
cha mwaka 2012/2013 watalii kutoka nje waliongezeka hadi 14,299 na wa ndani
walifika 9,994.
“Ni matarajio yetu idadi ya watalii
itaongezeka katika kipindi hiki cha 2013/2014; hiyo yote ni kutokana na mambo
mengi yanayofanywa katika kuitangaza hifadhi hii yenye upekee,” alisema.
Alisema hifadhi ya Taifa ya Ruaha ipo
katika eneo linalokutanisha ukanda wa kaskazini mashariki na kusini mashariki
mwa Afrika na hivyo kuifanya iwe na aina mbalimbali za mimea na wanyama ambao baadhi yake hawapo katika hifadhi
nyingine.
Aliwataja naadhi ya wanyama
wanaopatikana katika hifadhi hiyo kuwa ni pamoja na idadi kubwa ya tembo kuliko
hifadhi nyingine yoyote Afrika Mshariki, aina 571 ya ndege wakiwemo wale
wanaozunguka nchi mbalimbali, swala, tandala mdogo na mkubwa, samba, nyati,
pundamilia, twiga, boko, mamba, chui, mbwamwitu,
nyani, mbwea na wengineo wengi.
Alisema katika hifadhi hiyo, wanafanya
utali wa usiku ambao husaidia watalii kuona wanyama wasioonekana mchana, utalii
wa kutembea kwa miguu ili kumfanya mtalii awe jirani na mazingira ya hifadhi na
utalii wa masafa marefu kwa kutumia magari.
1 comment:
wanataka kuja kuwachukua wanyama hawa na kuwapeleka makwao wanaona nyinyi waafrica hamustahili kuwa nao hajui kuwatunza mnawatesa hawa wanyama bora wakakae katika ma zoo yao waingize pesa na watoto wao wawaone wanyama hawa mpoooo.kama hampo laleni usingizi
Post a Comment