Picha ya video inayomuonesha msanii Justin Bieber akitumia neno la kibaguzi dhidi ya watu weusi imepatikana na gazeti moja.
Picha hiyo iliyopatikana na gazeti la The Sun, ilipigwa mwaka 2011 wakati wakitengeneza filamu yake ya 'Never Say Never'.
Picha hiyo inamuonesha Bieber akiwa kwenye kochi na
Mwimbaji huyo ambaye umri wake sasa ni miaka 20 anamalizia sentensi yake kwa kufanya mlio wa msumeno na kisha kutumia neno la kibaguzi mara tano.
Gazeti hilo linadai kuwa baadhi ya watu wa karibu wa Bieber wamekuwa wakijaribu kuficha picha hiyo ya video kuonekana hadharani.
Tovuti ya Newsbeat ya BBC ilijaribu kuwasiliana na mwimbaji huyo kwa simu na barua pepe, lakini hakuna jibu lolote lililopatikana hadi sasa.
Bieber amekuwa na mwaka wenye misukosuko.
Jaji wa mahakama moja mjini Florida aliahirisha kesi yake ya tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa, hadi mwezi Julai.
Mwimbaji huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari na leseni iliyopita muda wake na kugoma kukamatwa na polisi.
Bieber pia anakabiliwa na mashtaka nchini Canada ya kumshambulia mtu kwa kumpiga kichwani.
Pia, nyumba yake ilipekuliwa na polisi mwezi Januari, baada ya kutuhumiwa kusababisha hasara ya maelfu ya dola katika nyumba ya jirani yake baada ya kuishambulia kwa kurusha mayai.
2 comments:
kutumia msumenono ndo nini tena hebu tujuzuni waugwana kiswahili siku hizi kina maneno mengi
kipi cha ajabu wazungu siku zote wana zarau kwa watu weusi na sisi bado tu tunawanganania utafikri malaika wao kipi cha ajabu hasa hasa huku marekani ndo kuna ugabuzi kuliko hata ujerumani alipokuwa hitler enzi zake
Post a Comment