
MTU mmoja amefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Ukerewe, Mwanza kwa tuhuma za kukutwa akifanya mapenzi na mbuzi.
Mtuhumiwa
huyo, William Sebastian (21), mkazi wa Kijiji cha Mlezi alisomewa
mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya hiyo,
Faustine Kishenyi.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, Inspekta Samwel Onyango aliieleza mahakama hiyo
kuwa mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 4 mwaka huu saa 9 alasiri
huko Mlezi, Ukerewe.
Katika
hati ya mashitaka imeelezwa kuwa mshitakiwa huyo alikutwa akitenda kosa
hilo katika banda la mbuzi nyumbani kwao na mmoja wa wanafamilia.
Katika
maelezo hayo, Onyango alisema mwanafamilia huyo ambaye ni mwanafunzi wa
darasa la tatu katika Shule ya Msingi Mlezi, baada ya kushuhudia tukio
hilo alikwenda kutoa taarifa kwa baba yao, Maxmilian Stephan aliyefika
na kumkuta mtuhumiwa akiendelea `kuhangaika’ na mbuzi huyo.
Akifafanua, alisema kosa hilo ni kinyume cha sheria ya makosa la kujamiiana kifungu namba K/F 154 (1) na (2) C sura ya 16 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002. Mtuhumiwa amekana kutenda kosa hilo na amerudishwa rumande kwa kukosa wadhamini
No comments:
Post a Comment