Advertisements

Saturday, June 7, 2014

WAKAZI WA KITONGOJI CHA ZAHANATI KIJIJI CHA IGURUSI WILAYA YA MBARALI MKOANI MBEYA WACHUSHWA NA DAMPO LA TAKA LILILOPO KARIBU NA MAKAZI YAO.




               Hilo ndilo dampo linalolalamikiwa na wakazi hao





Huyu bibi ni mmoja kati ya wakazi ambao nyumba zao zipo karibu na dampo hilo pamoja na huyo mzee aliyesimama pia huyo mzee alikuwa akifanya biashara ya bucha.

                   Diwani wa kata ya Igurusi Mh, Keneth Ndingo

 

Wakazi wa kitongoji cha Zahanati kijiji cha Igurusi wilaya ya mbarali mkoani Mbeya wameulalamikia uongozi wa serikali ya kijiji hicho kwa kushindwa kuondoa kwa wakati  taka zilizopo katika dampo ambalo limejengwa karibu na makazi ya watu.

 

Wakiongea na blog hii wakazi hao wamesema tangu kujengwa kwa dampo hilo yapata zaidi ya miaka nne sasa serikali haijawahi kuondoa taka hizo na kuzimaliza isipokuwa imekuwa ikiziondoa na kuzibakiza.

Kufuatia hali hiyo ndio imekuwa chanzo kikubwa cha kujaa kwa haraka kwa dampo hilo hivyo kusababisha taka kuzagaa mpaka katika makazi yao ambapo huwapa kero kubwa katika kufanya kazi zao kutokana na harufu mbaya inayotoka katika dampo hilo.

 

Aidha wamesema eneo hilo miaka ya nyuma walikuwa wakifanya biashara mbali mbali ikiwemo chakula na mabucha ya nyama ya ng’ombe hivyo tangu kujengwa kwa dampo hilo ufanyaji wa biashara umekuwa ni mgumu kutokana na taka zinazotupwa katika dampo hilo hivyo wafanya wafanyabishara hao kuamua kuondoka na kwenda kutafuta sehemu nyingine za kufanyia bishara zao.

 

Hata hivyo wakazi hao wameiomba serikali kuondoa dampo hilo kutokana na kushindwa kuondoa taka hizo ili wao waendelee na shughuli zao za kujitafutia kipato. 

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa kijiji hicho Mussa Mwanjejele amekiri kuwepo kwa hali hiyo na kusema sababu ya kuchelewa kwa uondoaji wa taka hizo ni halmashauri kuchelewa kutoa fedha kwaajili ya kuondolea taka hizo.

 

Amesema mpaka kufikia kuondoa taka hizo ni lazima wakapige  kelele halmashauri ndipo wapewe fedha za kuondola taka lakini bado fedha wanazopewa hazikidhi uondoaji wa taka zote hivyo kusababisha taka zingine kubaki katika dampo hilo.

No comments: