Advertisements

Monday, June 16, 2014

MBASHA NA MKEWE FROLA KUMBE WANA LAANA YA ASKOFU KULOLA

SAKATA la tuhuma za ubakaji zinazomkabili mume wa Flora Mbasha sasa limechukua sura mpya baada ya maovu yao mengine kuanikwa hadharani na ndugu wa Flora…..

Msichana mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Cathy ambaye ni dada binamu wa Flora amedai kuwa kinachowatafuna wawili hao ni laana waliyoipata kutoka kwa babu wa Flora, marehemu baba Askofu Moses Kulola…..
Ndugu huyo wa Flora amesema kuwa wawili hao waliwahi kufikia nyumbani kwa askofu Kulola huko Mwanza,siku chache kabla ya Kulola kuaga dunia na kufanya madudu mengi ikiwemo kuingiza askari polisi kwenye chumba cha Kulola.

Ndugu huyo alidai kuwa wawili hao walifikia hatua ya kuingiza askari kwenye chumba cha askofu Kulola kwa madai ya kuibiwa sh. 300,000 ( Laki tatu ) za Emmanuel Mbasha, mume wa Flora huku wakimwaga matusi mazito kwa wajukuu wa Kulola….

“Walifikia pale kwa babu, yule Mbasha akawa na pesa kama laki tatu hivi, akazihifadhi kwenye nyumba ndogo ya chini waliyofikia,nyuma ya nyumba ya babu, akawa amesahau alikoziweka zile pesa basi wakaanza kuwatukana matusi ya nguoni wajukuu wa babu pale kama hawana akili nzuri, yeye Mbasha na Flora,” alisema ndugu huyon wa Flora.

Akaendelea kudai kuwa walipoona hakuna ushirikiano kwa wajukuu wa babu wakaamua kuita polisi waliofika pale nyumbani na kuanza kufanya upekuzi wa nguvu kwenye kila kona ya nyumba ya baba Askofu….

“Walipoona hawajafanikiwa kuzipata akaamua kuwaingiza polisi mpaka chumbani kwa babu, na babu alikuwa hayupo nyumbani, alikuwa kanisani, sasa aliporudi ndipo alikuta askari chumbani kwake wakifanya upekuzi. Babu alikasirika sana na kujikuta akimwaga machozi,” alisema Cathy

Akaendelea kudai kuwa babu alishangaa sana kufikia hatua ya wawili hao( Flora na mumewe) kutomwamini hata yeye mpaka kuingiza askari ndani ya chumba anacholala lakini wawili hao walimpuzaa hata baba Askofu huyo….

“Babu aliwalaani wale na aliwaambia kuwa siku si nyingi maovu na uchafu wao utajulikana kwenye jamii huko Dar wanakowaibia watu kwa kujifanya wameokoka wakati siyo kweli na wanatapeli watu kila siku,akasema wataishia pabaya muda si mrefu,” alisema Cathy.

Akaendelea kudai kuwa Flora na mumewe hawakuwahi kuomba radhi kwa babu yao Askofu Kulola mpaka alipofariki, na mpaka leo hii laana yake bado inaawatafuna sana na haya yanayoendelea ni matokeo ya laana hiyo.
CREDIT:USPESHO

2 comments:

Anonymous said...

Mh! Udaku at its best ...

Anonymous said...

khaaaa! Mweee! Mie simo!