Advertisements

Monday, June 16, 2014

MSAKA PESA TOKA MACHAME ALIYEISHIA KWA MATAPELI WA MAPENZI JIJINI DAR

Jackline Wolper ni mmoja kati ya warembo wenye umaarufu mkubwa nchini na katika soko la Filamu za Tanzania.

Anamvuto unaokubalika na wengi na ameweza kujipatia umaarufu mkubwa sana kupitia filamu alizoshirikishwa na alizozifanya chini ya kampuni yake mwenyewe. Pia ni mwandishi mzuri wa Script na muongozaji mzuri wa filamu....

Alizaliwa Moshi mkoani Kilimanjaro na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Mawenzi huko huko Moshi.Baadae alipata elimu ya sekondari katika shule ya sekondari Magreth Ekenywa iliyopo jijini Arusha na inasemekana aliendelea na masomo nchini Kenya.....

Rekodi zinaonyesha kuwa alitua jijini Dar kati ya mwaka 2005 na 2007 akiwa na jukumu moja tu la kusaka pesa.Kama ilivyo ada kwa jamii ya watu wa kabila lake baada ya kufika jijini Dar hakulaza damu, fasta alicheki michongo ilipo na kuanza kuifanyia kazi..

Kujulikana kwake kulianzia pale alipoanza kupita mitaani akitembeza bidhaa za mikononi na kuziuza kwa bei ya promosheni. Hakuna aliyejua machina Wolper angekuja kuwa bonge la staa nchini Tanzania...
Ni kipindi hiki ambacho wanaume walimchukulia poa na kumpita bila hata salamu kama vile wafanyavyo kwa kina dada wanaotembeza bidhaa za mikononi.Ni wanaume wachache sana ndo waliweza kugundua uzuri wa Wolper na kumtupia maneno mawili matatu yenye ushawishi wa ngono....

Baadae aliingia kwenye biashara za Saluni maeneo ya Tandale jijini Dar kabla ya kujiingiza kwenye sanaa ya uigizaji....

Kipindi flani Wolper akiishi maeneo ya Mwenge alikutana na mtu mmoja wa kabila lake aliyefahamika kwa jina la Injia Macha ambapo jamaa huyo alianzisha utani wa kumuita mjomba lakini baadaye ujomba ukapitiliza na akaanza kuomba kulila tunda....

Inasemekana kwamba jamaa alifanikiwa kulila tunda kwa kipindi kirefu na aliponogewa alimuhamisha Wolper toka Mwenge alikokuwa akiishi na dada yake na kumpangishia chumba cha kwanza maeneo ya Sinza Mori....

Injinia huyo alimpatia Wolper gari chakavu aina ya Toyota Celica ambapo baada ya siku kadhaa Wolper aliipiga bei gari hiyo.....

Akiwa mitaa ya Sinza ndipo akakutana na mwanadada Lucy Komba ambaye ni msanii wa filamu aliyemshawishi kujiingiza katika tasnia hiyo....Kipindi hicho ilikuwa ni mwaka 2009.

Baada ya kupata mtonyo wa Movie, Wolper aliuchangamkia na kwa mara ya kwanza akaonekana katika filamu ya 'Ama Zangu Ama Zao' iliyofanywa na mwanadada Lucy Komba...

Baada ya hapo alianza kupata mialiko toka kwa watu mbalimbali ili aweze kuigiza kwenye filamu zao.Alifanikiwa kukutana na Director mkongwe,William Mtitu na marehemu Steven Kanumba na kufanya filamu mbalimbali zilizomjengea jina katika tasnia hiyo....

Baada ya kuanza kupata mafanikio, Wolper alizinguana na Injia Macha ambaye alikuwa amempatia gari nyingine aina ya Toyota GX 100....

Mgogoro mkubwa uliibuka kiasi cha Injia Macha kuwatumia polisi kumnyanga'anya gari hilo Wolper.Polisi walimkuta akiwa na gari hilo maeneo ya Ilala ambapo alielezwa kuwa gari hilo linatafutwa na mwenyewe na lina kesi katika kituo cha polisi Oysterbay.

Wolper akiwa hajui kama mchongo huo ume injiniwa na Injia Macha alitaka kuwavimbishia kifua maafande akidai kuwa gari hilo alinunuliwa na mjomba wake na kadi anazo.Lakini alijikuta akigonga mwamba kuondoka na gari hilo pale polisi walipomtaka waende kituoni kulihifadhi gari hilo kisha akamlete huyo mjomba wake pamoja na kadi za manunuzi ya gari hilo...

Wapekenyuzi wanaeleza kuwa kipindi hicho tayari Wolper alikuwa na bwana mwingine na Injia Macha alishaushtukia mchongo na ndio sababu alimfanyia umafia bila Wolper kujua....

Wolper akaingia mkenge, akamshtua bwana'ke mpya kuhusu polisi wanachotaka kukifanya.Bwana'ke akamwambia asijali, wakutane Oysterbay Polisi ili akalichukue hilo gari mbele ya maafande....

Kilichotokea ni kwamba baada ya Wolper kufikia kituo cha Polisi alivutwa sikio na afande mmoja kwamba Injinia Macha yupo kituoni hapo na anawasubiri kwa hamu yeye na bwanake waje na documents za umiliki wa gari hilo hali iliyomfanya Wolper aingie mtini....

Inasemekana kuwa kama bwana mpya wa Wolper angetokea kituoni hapo angetiwa ndani yeye na Wolper kwa kesi ya wizi wa gari lakini machale yakawacheza wakalala mbele.....

Baadaye Wolper alisikika kupitia Radio Clouds FM akitangaza kuwa amedhulumiwa gari na mjomba wake ambaye alimuongezea pesa kidogo katika manunuzi ya gari hilo lakini baadaye akawa anamtaka kimapenzi na kumzushia kwamba amemuibia gari. Huu ndo ukawa mwisho wa Wolper na Injia Macha.

Baada ya kutemana na Injia Macha, Wolper alipitia kwenye mikono mingi ya kimahusiano lakini uhusiano mwingine uliompandisha chati ni ule wa Abdallah Mtoro almaarufu Dallas....

Dallas akiwa hana jina la kutosha ndani ya jiji la Dar es Slaam, ghafla alikuwa maarufu baada ya kutangaza ndoa na Wolper na hasa pale alipompatia kiasi cha Dolla elfu 10 ( Tsh 16 Milioni) akampatie marehemu Sajuki kwa ajili ya matibabu. Kitendo hicho kilimfanya Wolper awafunike mastaa wote wa kike akiwemo Wema Sepetu......
Hata hivyo mahusiano ya Dallas kwa Wolper yalijaa utapeli mwingi kwani wakiwa bado hawajafahamiana na Dallas ambaye inasemekana ni mfanyabiashara wa 'Sembe' alimuingia kimafia Wolper na kufanikiwa kumteka kimapenzi hadi akafunga naye ndoa.....

Umafia alioufanya Dallas ni pamoja na kumpenyezea vitu vya thamani kama vile magari ya kifahari na pesa za matumizi.

Kwa kuwa Wolper tangu anatoka Machame alijua anakuja mjini kutafuta pesa, hakupoteza muda kutaka kujua mambo mengi kuhusu Dallas. Alichoaangalia ni Dallas amekuja na mkono gani? Mkono mtupu, mkono wa birika au mkono wa madini?

Alipogundua kwamba jamaa alikuwa na madini ya kutosha akajitoa mzima mzima na kumkabidhi Dallas moyo wake wote , mwisho wa siku akajikuta akiumbuka na kuambulia maumivu baada ya kumtambua Dalls ni mtu wa namna gani.

No comments: