Advertisements

Monday, June 16, 2014

MZEE MPONDELA "CASTRO" KUZIKWA KWAO TABORA JUMATANO

RAMBIRAMBI:
Uongozi wa klabu ya Young Africans unatoa pole kwa familia ya marehemu George "Castro" Mpondela aliyewahi kua Katibu Mkuu wa Yanga SC mwanzoni mwa miaka ya tisini aliyefariki usiku wa kuamkia jana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaaam.

Marehemu aliwahi kuwa Katibu mkuu wa Yanga SC wakati wa uongozi wa mwenyekiti Abbas Gulamali na mpaka umauti unamfika usiku wa kuamkia jana alikua akisumbuliwa na matatizo ya Shinikizo la Damu


Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu Dickson George Mpondela, msiba upo nyumbani kwa marehemu Mnarani- Makaburini (Magogoni) Kigamboni na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Alhamisi jijini Dar es salaam.

Yanga SC inatoa pole kwa familia ya marehemu, wanachama, wapenzi na wadau wa soka kwa ujumla popote pale walipo.

Bwana Ametoa na Bwana Ametwaa Jina la Bwana Lihimidiwe. 
Amen

No comments: