Hawa ndio Tano Ladies ambao hufanya maajabu kila mwaka na kujaribu kuwaweka wakina mama karibu kwa kuwaletea watu mbalimbali wenye mawazo tofauti ya maendeleo ya kumkwamua mama ili asiwe tegemezi kwa mumewe na aweze kuleta maendeleo kwenye familia na jumuiya inayomzunguka kwa kuamini kwamba maendeleo ya mama ndio maendeleo yanayoleta mabadiliko ya haraka na yanayoonekana kwa kuamini kwamba mwanamke ndiye kioo cha Dunia. Kutoka kushoto ni Asha Hariz, Justa Mtalemwa, Iska Jojo, Asha Nyang;anyi na Tumaini Kaisi
Ify Anne Nwabukwu ambaye ni Rais wa African Women's Cancer Awereness Association(AWCAA) akiwaeleza wanawake jinsi gani ya kuweza kujitambua na kugundua mabadiliko mwilini mwao na kwenda sehemu husika ya kuangalia, kupima na hatimae kupata matibabu kama utagundulika na kuwaeleza akina baba wawe kioo cha akina mama kama watagundua mabadiliko yeyote kwenye mwili wao wawajulishe mapema kwani mabadiliko hayo inaweza ikawa ni ugonjwa wa Saratani.
Maxiwell Akinsehiwa ambaye ni Mkurugenzi masoko wa kampuni ya Pacific Life akiwaeleza wahudhuriaji kwenye Tano Ladies Mingle Night njia iliyobora kwa maisha ya Marekani na kuwatahazarisha wadau kuwa makampuni mengi hutoa huduma kwa kutoweka wazi huduma zao kwa maswala muhimu ambayo mwananchi hususani wageni wanaokuja nchini Marekani ambao hawaelewi mabo yanavyokwenda. Maxiwell aliendelea kusema makampuni mengi yanayotoa huduma za Bima ya Maisha, huduma za kibenk yanaaga,ia faida zaidi kwa vitu kama vile inabidi kuwa makini au kumtafuta mtaalam atakayekuelezea na kukufafanulia zaidi bila hivyo utajikuta maisha yako ya uzeeni yakiwa mgumu sana.
Zawadi Ukondwa nae akielezea jinsi gani alivyomstali wa mbele katikakusaidia na kuchangia maendeleo ya akina mama huku akiagalia zaidi nyumbani Tanzania na kusisitiza ni vizuri kwenye maisha chochote unachopata japo kidogo kujaribu kusaidia wengine hasa kwenye Jumuiya inayokuzunguka huku akielezea jinsi gani alivyoweza kusomesha watoto waliokuwa wakihitaji elimu ambao hawakua na uwezo.
Hariett Shangarai wa Nesi Wangu akielezea jinsi gani anavyosaidia Jumuiya na kuwezesha kusomesha watoto mkoani Kilimanjaro nchini Tanzania yote ni kwasababu anakumbuka alikotoka na maisha aliyopitia na husaidia jumuiya ya DMV kwa kutoa uashauri wa utabibu na kuleta madakitari wanao toa huduma bure kwa ajili ya kusaidia Jumuiya ya Watanzania.
Miriam mwenye kitabu cha Taste of Tanzania kinachoelezea na kufundisha mapishi ya vyakula vya Kitanzania nae akielezea jinsi ya kumkomboa mwanamke bila kuwa tegemezi wa rushwa ya ngono huku akimsifia Haika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden Hotel Ltd aliyekuja kutoka Tanzania na kutoa mada ya jinsi gani mwanamke unavyotakiwa uwe jasiri wa kutafuta njia za kuweza kujikwamua kimaisha badala ya kupoteza muda wa kujipara ili umpendezeshe mwanaume badala yake unaweza kufanya kinyume, uwe jasiri, mwadilifu na bila kuwa mwoga wa kujichanganya na watu wengine kwa kufanya hivyo ni kujaribu kupata mawazo tofauti na mbadala wa mambo mengine yaliyokuwa yakikukwamisha katika maisha au biashara zako.
Kulia ni Haika Lawere mmiliki wa Mbezi Garden Hotel Ltd aliyekuja toka Tanzania kwa sherehe za miaka miwili ya Tano Ladies ambazo leo zinafikia kilele kwa Gala Dinner itakayofanyika Martin's Crosswinds, Greeenbelt, Maryland. na Balozi wa Tanzania nchini Marekani ndiye atayekuwa mgeni rasmi, kushoto nia Mama yake Zawadi Ukondwa na Zawadi.
Wahudhuriaji wakifuatilia jambo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
1 comment:
Tunawapendaje kina mama zetu mliokuja kutusupport??? kutoka kushoto picha ya mwisho Mama Safari, Mama Nyang'anyi, Mama Kombe, Mama Ukondwa, Mama Mukami, Mama Mushi, Mama babe Mgaza!!
Mungu awape umri mrefu na afya tele! Amina
Post a Comment