Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akizungumza na Mhe. Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaoendelea Jijini London, Uingereza.
Kwenye sherehe za ufunguzi, waandaaji wa mkutano huo walisifia nchi zinazochangia kuleta amani kwenye maeneo yenye migogoro duniani . Aidha walisifu hatua ya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za kwanza kukubali na kusaini Tamko la Umoja wa Mataifa la Kukomesha udhalilishaji wa Kijinsia katika maeneo yenye migogoro. (Declaration of Commitment to End Sexual Violence in Conflict).
Waandaaji wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro, Mhe. William Hague, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza na Bi. Angelina Jolie, Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Wakimbizi, wakitoa hotuba zao za ufunguzi kwenye mkutano huo unaoendelea Jijini London, Uingereza.
Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiweka saini hati ya tamko la jumla la mkutano huo likiwataka washiriki kuchukua hatua sasa ya kukomesha udhalilishaji wa kijinsia kwenye maeneo yenye migogoro.
Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Ukomeshwaji wa Udhalilishaji wa Kijinsia kwenye Maeneo yenye Migogoro unaondelea Jijini London, Uingereza. kuanzia tarehe 11 hadi 13 Juni, 2014.
No comments:
Post a Comment