ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 12, 2014

MKUU WA WILAYA YA SPRINGFIELD SAFARINI MAKKAR NA MADINA


 Mkuu wa wilaya ya Springfield. MA Bwana Isaac Kibodya na mama mwenye nyumba wake wakiwa Makkar. Makkar na Madina ni miji takatifu duniani ni sehemu ambayo  waumini wa kiislam kutoka duniani kote ufika hapa kwa ajili ya swala ya Umrah inayofanyika kila mwaka. Kwa wale waumini wa dini ya kiislam wanaelewa maana yake.  


5 comments:

Anonymous said...

Ni Ibada kaka sio hivyo kua na stara ibada nzuri hufanywa kwa siri mungu akujaalie ila sio vema kujiachia ibadani km hv

Anonymous said...

DJ Luke naona umekosa mwelekeo kabisa na dira nzima ya blog yako, huyu jamaa siyo mkuu wa wilaya wala lolote lile, hawa watu wanapenda kujitangaza kwa sababu wameshindwa maisha. Naoan wanakulipa ili kuwatangaza. Ungekuwa unatangaza mambo ya kusaidia jamii naona hilo lingekuwa jambo zuri sana.
Hata wewe huna sera na utangazaji wa blog yako iko upande mmoja.

Nina hakika hutayaweka maoni yangu kwa hiyo kazi kwako. Ulianza vyema lakini sasa umepotoka kabisa.
Usipogeuza mwelekeo naona blog yako mwisho wake uko karibu.

Anonymous said...

mashallah na sisi tuombeeni inshallah Allah atujaliye tuweze kufanya safari hii inshallah

Anonymous said...

Wewe anonymous number mbili unaposema hawa watu wameshindwa maisha wewe ndio unayewaendeshea maisha yao??ibada tangu lini ikawa siri???kama ingekuwa siri basi viongozi wetu wa dini wasingekuwa wanatuhamasisha kumuabudu Mungu, wewe unaonekana una chuki binafsi kama huna cha kucoment ni bora ungekaa kimya, unaposema wamezoea kujitangaza waliweka mabango ya matangazo kujitangaza??acha chuki binafsi mwenzio akifanya jambo jema basi muombee mema sio kuropoka hovyo tuu. Huyu bwana amefanya jambo zuri ambalo ni mfano mzuri wa kuigwa ili na sisi wengine Mungu atujaalie tuweze kuiga mfano wao. Big up brother Mungu azidi kuwaongoza katika maadili mema ya kidini.

Anonymous said...

Kweli kabisa ndugu yangu mimi mwenyewe hawa jamaa wamenihamasisha sana namuomba Mungu aje kunijaalia na mimi na familia yangu kama hatukuweza kwenda Hija basi iwe Umrah na InshaAllah kwa uwezo wake Mungu nina imani nasi tutafanikiwa. Shukrani sana ndugu yetu bwana Kibodya kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa Mungu awakubalie ibada zenu InshaAllah