Mtoto Jeremiah Nyamuhanga (2) mkazi wa Machimbo amekufa baada ya kutumbukia kwenye kisima cha maji karibu na nyumbani kwao.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema, mtoto huyo
alitumbukia juzi saa 10 jioni katika eneo la Machimbo, Kitunda, Wilaya
ya Ilala.
Alisema
maiti yake ilikutwa ikielea ndani ya kisima hicho kilicho karibu na
nyumba yao. Inasadikiwa mtoto huyo alimtoroka baba yake aliyekuwa kwenye
banda la kuku na kwenda kucheza ambapo alitumbukia ndani ya kisima
hicho.
Maiti ya mtoto huyo amehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na upelelezi unaendelea

No comments:
Post a Comment