ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 7, 2014

KELELE ZA BAA, KLABU KUDHIBITIWA


Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), imetunga kanuni ya kudhibiti kelele na mitetemo kutoka kwa waendeshaji wa klabu za usiku, baa, matangazo ya wanaozunguka barabarani na hata mahubiri katika maeneo ya ibada.
Kwa sasa kanuni hiyo iko kwa Mchapishaji Mkuu wa Serikali na tayari imesainiwa na
Waziri anayeshughulikia Mazingira. Kadhalika wananchi wametakiwa kutoa taarifa za kero zitokanazo na maeneo hayo ya biashara kwani yamekuwa yakichangia kuporomosha maadili ya taifa.
Mkurugenzi wa Uzingatiaji na Utekelezaji kutoka Baraza la Mazingira nchini (NEMC), Dk Robert Ntakamulenga alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia kero ambazo wananchi wamezifikisha ofisini kwake.
“Kama unapiga kelele inayozidi kiwango cha desbell 45 inahitajika kibali na kelele za aina hiyo ni zile zinazoanzia saa moja asubuhi hadi saa nne usiku iwe mwisho,” alisema na kuongeza baa ambazo zinapiga kelele za aina hiyo hadi usiku zinavunja sheria,” alisema Ntakamulenga.

1 comment:

Anonymous said...

Saws kabisa nakubaliana na hilibswala ni mujimu sana kwabkuwapa fursa watu kutulizana mawazo na pressure za kazi na foleni. Itifaki izingatiwe.