Kamati
ya Uchaguzi wa viongozi wa jumuiya ya Watanzania DMV inapenda kuwakumbusha
wanajumuiya kuwa leo June 6, 2014 saa sita usiku ndiyo mwisho wa kurudisha fomu
kwa wale wanaotaka kugombea uongozi katika Jumuiya.
Kamati
hii inawataka kuwakumbusha utaratibu wa kupiga kura kama ulivyotangazwa kwa
mujibu wa katiba:
1)
Kamati itatangaza
majina ya wagombea waliowapitisha na wagombea hao kuanza kampeni.
2)
Tarehe ya
uchaguzi ni juni 21 na kama kutakuwa na mabadiliko tutawatangazia.
Tunaomba uje na kitambulisho au aina yoyote ya ID
ili uweze kutambulika kama mpiga kura halali.
No comments:
Post a Comment