AFISA HABARI WA TCRA INNOCENT MUNGI AKITOA TAARIFA YA UZINDUZI WA MITAMBO YA KIDIGITALI ILIYOFUNGWA HIVI KARIBUNI MJINI KAHAMA.
Halmashauri tatu za
wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga zimetakiwa kuutumia Mtandao wa kurusha matangazo kwa mfumo wa Dijitali uliozinduliwa mjini Kahama kwa kuanzisha kituo cha televisheni cha wilaya
Wito huu umetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na kaimu mkurungezi wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Habby Ngunze wakati wa uzinduzi wa mtambo huo wa kurusha matangazo ya dijitali uliofanyika mjini Kahama
Katika uzinduzi huo Ngunze amesema kwa kutumia mtambo huo Wilaya ya Kahama ni kwanza Tanzania kuingia moja kwa moja kwenye dijitali bila kupitia analojia kati ya wilaya nyingine 136 zilizopo hapa nchini ambazo hazijapata huduma hiyo
Kufuatia hali hiyo Ngunze ameitaka serikali wilayani Kahama kupitia halmashauri zake tatu za mji ushetu na Msalala kuhakikisha zinaanzisha kituo cha televisheni hali itakayonufaisha wananchi wote wa wilaya hiyo ambayo wataweza kupata habari zao kwa kiwango kizuri
Naye Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya amesema atakaa na wakurungenzi wote watatu wa halmashauri zake pamoja na waandishi wa habari waliopo mjini Kahama ili kujadiliana kuona uwezekano wa kuanzisha kwa kituo hicho cha televisheni ya jami
No comments:
Post a Comment