NIGERIA
imeitoa kimasomaso Afrika baada ya kufuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe ka
Dunia, licha ya kufungwa mabao 3-2 na Argentina katika mchezo wa Kundi F
uliofanyika Uwanja wa Beira-Rio mjini Porto Alegre, Brazil.
Nigeria
imemaliza na pointi nne katika nafasi ya pili nyuma ya Argentina yenye
pointi tisa, hivyo kuwa timu ya kwanza ya Afrika kufuzu 16 Bora.
Lionel
Messi alianza kuifungia Argentina bao la kwanza dakika ya tatu, lakini
Ahmed Mussa akaisawazishia Super Eagles dakika moja baadaye.
Messi
tena akaifungia Argentia bao la pili dakika ya mwisho ya kipindi cha
kwanza kabla ya Mussa tena kuisawazishia Nigeria dakika ya ya pili baada
ya kipindi cha pili.
Marcos Rojo aliihakikishia Argentina ushindi wa mechi zote za Kundi lake baada ya kufunga bao la tatu dakika ya 50.
Bosnia
imeifunga mabao 3-1 Iran na kumaliza katika nafasi ya tatu kwa pointi
hizo tatu, wakati Iran yenye pointi mbili imeshika mkia.
Ivory
Coast na Cameroon zote tayari zimeaga na timu nyingine za Afrika zenye
nafasi ya kwenda Raundi ya pili ni Algeria na Ghana, iwapo zitashinda
mechi zao za mwisho.
Kikosi
cha Argentina kilikuwa; Romero, Zabaleta, Federico Fernandez, Garay,
Rojo, Gago, Mascherano, Di Maria, Messi/Alvarez dk19, Higuain/Biglia
dk90 na Aguero/Lavezzi dk37.
Nigeria; Enyeama, Ambrose, Yobo, Oshaniwa, Omeruo, Odemwingie/Nwofor dk80, Onazi, Mikel, Babatunde/Uchebo dk66, Musa na Emenike.

Nyota: Lionel Messi (juu) amefunga mabao mawili Argentina ikiifunga Nigeria 3-2 leo
No comments:
Post a Comment