Mamlaka
nchini Saudia Arabia ipo kwenye zoezi la kupima chokleti za Cadbury
zinazotengenezwa Uingereza kufuatia kashfa juu ya kuwekwa kwa
virutubisho vya nyama ya nguruwe kwenye bidhaa hizo kugunduliwa nchini
Malaysia ambapo wito wa mgomo uliotolewa kwa makampuni yanayodhalisha
bidhaa hiyo.
Siku chache zilizopita Mamlaka nchini Malaysia iligundua
uwepo wa nyama za nguruwe kwa kutumia DNA katika bidhaa hiyo ya Cardbury
Daily Milk huku taarifa ikimnukuu makamu wa Rais wa sekta ya
Chakula(SFDA) akisema kwamba kufanya vipimo hakukuhusisha bidhaa
nyingine za Cardbury zinazozalishwa katika viwanda vya Malaysia na
zilikuwa zikiagizwa kutoka nchi nyingine kama vile Misri na Uingereza.
Ijumaa iliyopita Taifa la Indonesia lenye wakazi wengi
waislamu nao pia walikuwa wakipima bidhaa hizo kwa kuangalia kama
zinazingatia vigezo vya kiislamu. Kashfa ya masharika yanayotengeneza
vyakula visivyo halali ilianzia kusini mwa bara la Asia ambapo mwaka
2001 baraza la maulamaa la nchini Indonesia liliishtaki kampuni kubwa ya
kijapani Ajinimoto iliyokuwa inatengeneza bidhaa za kula kwa kutumia
virutubisho vya nyama ya nguruwe.
2 comments:
na ndo maana wanaipiga vita Malaysia na kutaka kuwaangamiza kwa vile kuna idadi kubwa ya waislamu wenye kuifuata dini yao na wala hawana mchezo mchezo na dini yao. mungu akubarikini sana wamalaysia.
na hizi ni mbinu ambazo wanazitumia sana katika sehemu walizo waislamu .mungu kiswawaona kishawamulika na njama zao.
rekebisha kichwa cha habari ni Malaysia ukisoma habari.
Post a Comment