ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, June 29, 2014

Snura Majanga Alia na Rushwa ya Ngono.....


\
Msanii wa muziki na filamu Snura Mushi amebainisha kuwa rushwa ya ngono kwa wanawake ni kikwazo kikubwa kinachowakwamisha wanawake kutimiza ndoto zao...
Snura aliamua kungukia suala hilo ili kuwatetea wanawake wanaoombwa rushwa ya ngono ili kupewa kazi, kwa kusema ni kitendo cha kinyama kwani wengi wanakuwa ombaomba kwa sababu tayari wamekosa kazi kutokana na kulazimishwa kitendo hicho.....

"Wanawake wanaweza lakini wengi wanakatishwa tamaa na baadhi ya watu wanaotumia nafasi zao vibaya. Unakuta mwanamke kafanya vizuri na ana uwezo mkubwa lakini suala la rushwa ya ngono ndo linalowavunja nguvu na kujikuta wakiwa tegemezi katika maisha yao," alisema Snura.

No comments: