ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, June 12, 2014

TAAAAAAAAANANIA TANZANIAAAAAA NA KUPENDA KWA MOYO WOTE

AJIRA UHAMIAJI USANII MTUPU.!!
Idara ya Uhamiaji nchini imetangaza nafasi za ajira. Imeita kwny usaili jumla ya watu 10,846 walioonekana wana sifa. Lakini wanataka watu 70 tu, kati ya waombaji wote hao zaidi ya 10,000 walioitwa kwenye usaili.
UNAELEWA HII INA MAANISHA NN??

Hii inamaanisha kuwa ni 0.64% tu ya walioitwa kwenye usaili watakaopata ajira, na 99.36% watatemwa. Huu ni wastani wa mtu mmoja kwa watu 156.
Hii ina maana kuwa kati ya watu 156 watakaosailiwa mmoja tu ndio ataajiriwa. Wakisailiwa wengine 156 mwingine mmoja aajiriwe. Huu si usanii jamani??
Mm nalaani sn mfumo huu wa kipuuzi uliotumika. Afu usaili wenyewe unafanyika Uwanja wa Taifa. Zaidi ya robo ya uwanja itajazwa na wahitimu hawa wa vyuo mbalimbali wanaohangaika kutafuta ajira usiku na mchana. Hii ni zaidi ya mashabiki wanaojitokeza kwenye mechi ya Yanga na Mgambo shooting.!
MY TAKE;
Serikali isitumie tatizo la ajira nchini kujitafutia umaarufu na kuwapa watu matumaini ya uongo. Hakukua na mantiki yoyote ya kuwaita watu wote hao wakati wanaotakiwa ni 70 tu. Hii ni janja ya nyani ya kujaribu kuwahadaa na kuwapa matumaini "feki" vijana hawa.
Ikumbukwe vijana hawa wanatoka mikoa yote ya Tanzania. wengine Mtwara, wengine Arusha, Mwanza, Kigoma etc. Wengine hawana ndugu Dar hivyo wamelazimika kushukia Guest. Wengine hawakua na nauli za kuja wamechangiwa na familia zao. Wengi ni watoto wa maskini ambao wazazi wao wanaishi chini dola moja kwa siku.
Hebu immagine mzazi ambae mwanae alifaulu kidato cha sita lakini hakupata mkopo kisa alichaguliwa kusoma course ambayo serikali inaziita "SIO ZA KIPAUMBELE". either Sociology, Mass communication, Rural development etc. Kwa kuwa alikosa mkopo mzazi akahangaika kumsomesha kwa nguvu zake. Kumlipia ada, na mahitaji mengine kama chakuka, malazi etc.
Akauza kila kitu cha thamani kwake ili mwanae asome. Akauza shamba, akauza mifugo na wakati mwingine akauza mazao ambayo ni akiba ya chakula nyumbani. Akadiriki kulala njaa ili mwanae asome.
Hatimaye mtoto amehitimu. Mzazi anategemea aanze kupata matunda ya nguvu zake lakini hamna ajira. Mtoto anakuwa mzigo kwenye familia. Halafu zinatangazwa nafasi za kazi UHAMIAJI. Nafasi zenyewe za "kisanii". Watu zaidi ya elfu 10 lakini wanatakiwa 70 tu.
Mzazi yuko Sumbawanga. Anaamua kuuza shamba mwanae aje mjini kujaribu bahati yake. hana mahali pa kushukia coz hana ndugu Dar. Analazimika kutafuta Guest ya bei rahisi kule Kigogo. Anajibanza hapo siku mbili tatu akijifua kwa ajili ya usaili.
Kisha anakwenda kwenye usaili anachujwa. Kisa walihitajika watu 70 tu kati ya zaidi ya 10,000 waliosailiwa. Immagine huyu mtoto anarudije nyumbani Sumbawanga. Atamweleza nn mzazi wake kama si kumuua kwa pressure??
SOLUTION.
Mi naamini serikali ina wataalamu wazuri tu inaoweza kuwatumia wakashauri juu ya mfumo bora wa usaili kuliko huu upuuzi uliofanywa na Idara ya Uhamiaji.
Ingeweza kufanyika namna flani ya Shortlisting na kupata watu wachache watakaoitwa kwenye usaili badala ya kumuita kila aliyeomba.
Kwa mfano kama walionba watu 10,000 wangeweza kufanya sorting kwa GPA. May be tunachukua wenye GPA kuanzia 3.0 na kuendelea. Hii ingefanya watu wenye GPA chini ya hapo wachujwe naturally.
Then waangalie vigezo vingine labda vipaumbele vya course. Kwamba tunataka waliosoma sheria 10 hivyo tuite kwny usaili 15. Tunataka Sociology 7 hivyo tuite kwny usaili 10. Baada ya kufanya shortlisting hii naamini ambao wangeitwa kwenye Usaili wasingezidi 100.
Na hii ingeleta maana halisi ya Usaili. Wakiitwa watu 100 wakati wanaohitajika ni 70 sio mbaya. Itz very reasonable. Lakini kuita watu 10,000 ili upate watu 70 huu ni wendawazimu. Ni upuuzi usiopaswa kuvumiliwa. Ni kuwabebesha watu mizigo isiyokua ya lazima.
Kwanza nadhani tumekuwa nchi ya kwanza duniani kuita kwenye usaili yeyote aliyetuma maombi.
Hivi wataalamu wa statistics waliojazana serikalini wanafanya kazi gsni?? Nawapa pole vijana wenzangu 10776 watakaochujwa kwny interview keshokutwa.
Na hao 70 watakaofanikiwa kupitishwa....naomba kudeclare interest mapema kuwa SITAKUA NA IMANI NAO. Kwa vyovyote hawa wameshaandaliwa tayari na wanajulikana. Hawa wengine 10776 wameitwa kusindikizwa tu ili isionekane wamepuuzwa.
NASISITIZA...
Si mbaya kumuita mtu kwenye usaili halafu akakosa kazi. Ila ni mbaya sana kumuita mtu kwenye usaili ukijua kabisa atakosa kazi.
Hii ni dhambi kubwa sana maana unamsimamisha mtu shughuli zake, unampotezea muda, unampotezea fedha huku moyoni ukijua kabisa hawezi kupata kazi. I hate this system.
Jipu limepasuka. siwezi kuwa adui kwa kusema ukweli.Hii ni "copy & paste" kutoka kwa Ndg. Malisa Godlisten Kama ni kweli basi kuna tatizo la msingi! ‪#‎Over‬.!!

No comments: