ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 10, 2014

UAMUZI RUFANI YA MICHAEL WAMBURA


UAMUZI RUFANI YA MICHAEL WAMBURA
Uamuzi kuhusu rufani ya Michael Wambura kupinga kuenguliwa kugombea urais wa Rais utatangazwa kesho (Juni 11 mwaka huu) saa 6 kamili mchana na Mwenyekiti wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF, Wakili Julius Lugaziya.
Boniface Wambura
Ofisa Habari na Mawasiliano
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
++++++++++++++++++++++++
HABARI ZA AWALI:
KOZI YA MAKOCHA YAZINDULIWA LEO DAR, AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Release No. 105
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Juni 10, 2014
KARIA KUFUNGUA KOZI YA MAKOCHA LEO
TFF_LOGO12Makamu wa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kocha ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Uzinduzi wa kozi hiyo ya wiki mbili utafanywa leo (Juni 10 mwaka huu) saa 6 mchana kwenye hosteli za TFF zilizopo Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam.
Makocha zaidi ya 20 wenye Leseni C kutoka Tanzania Bara na Zanzibar wanashiriki katika kozi hiyo inayoendeshwa na Mkufunzi wa CAF, Sunday Kayuni. Mkufunzi mwingine wa kozi hiyo anayetambuliwa na CAF ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi.
KANALI MWANAKATWE KUZIKWA LEO BABATI
Maziko ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wakati huo likiitwa FAT, Kanali mstaafu Ali Hassan Mwanakatwe yanafanyika leo (Juni 10 mwaka huu) Magugu, Babati mkoani Manyara.
Kanali Mwanakatwe alifariki dunia Juni 7 mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Jeshi (GMH) Lugalo jijini Dar es Salaam wakati akipatiwa matibabu baada ya kuanguka bafuni nyumbani kwake Mbezi Beach.
TFF imetoa ubani wa sh. laki tano kwa
familia ya marehemu Kanali Mwanakatwe, na katika maziko hayo inawakilishwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kanda ya Arusha na Manyara, Omari Walii.
AMBUNDO, SHIZA WATESA UHOLANZI
Wachezaji wa Tanzania walioko Uholanzi, Dickson Ambundo na Shiza Yahya wameanza kuonekana muda na waandaaji ya mashindano ya AEGON Copa Amsterdam.
Kwa mujibu wa wakala wa wachezaji wa Uholanzi, Denis Kadito, AEGON Copa Amsterdam ni mashindano ya kimataifa yanayoshirikisha timu kubwa kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni kwa wachezaji wa miaka chini ya 19.
Kwa Uholanzi, Ajax Amsterdam huwa lazima washiriki, na pia huwa kuna timu ya ridhaa inayotengenezwa kwa kuchagua “best talent” kutoka Uholanzi. Mchujo wa wachezaji hao kutengeneza timu ya kombaini, ulianza na wachezaji wasiopungua 1,000.
Kombaini hiyo inaitwa Men United na inafundishwa na mchezaji wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi, Ronald de Boer. Ronald e Boer ni pacha wa kocha wa Ajax (First team).
Ronald de Boer pia ni kocha wa wachezaji washambuliaji wa Ajax. Shiza na Ambundo waliingizwa kwenye mchujo na wakafanya vizuri, mwishoni wakaitwa kwenye timu ya wachezaji 18 waliotengeneza timu ya Men United. Hii ni mara ya kwanza wachezaji wasio Waholanzi kuingizwa katika timu hiyo.
Mashindano ya Copa Amsterdam yameanza juzi (Juni 8 mwaka huu) na yanaisha kesho (Juni 11 mwaka huu. Katika mashindano hayo kuna makundi mawili. Kundi A ni AFC Ajax (Amsterdam), Ajax Cape Town ( Afrika Kusini), Fluminense (Brazil), Hamburg SV (Ujerumani) wakati B ni Men United, Panathinaikos (Ugiriki), FC Aerbin (China) na Cruizero (Brazil).
Shiza na Ambundo wamecheza mechi zote tatu. Shiza amekuwa akicheza namba tatu wakati Ambundo anapiga namba tisa, saba na kumi na moja.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

No comments: