
Ujinga wetu wa kutotambua makusudi ya Mungu kukufanya mrembo, alikusudia kukurahisishia uonekane kwa urahisi na ili upate mume wa kukuoa.
Uzuri wako unautumia vibaya mwisho wa siku mnafanya kila kona ya mji mabango ya waganga wa kienyeji yaongezeke kukudanganyeni kuna dawa za mapenzi pia kukufanya uolewe.
Nakuuliza unakwenda kwa mganga ili uolewe nani kakuroga? Usinitumbulie mimacho kama dume la panya lililonaswa na mtego, nakuuliza wewe acha kuangalia pembeni.
Ulipokuwa ukipendwa hukutaka kuolewa, wanaume wakija unaona wanataka kukufuja kwani ule ndiyo wakati wako wa kuvunja mifupa ili uzeeni uwasimulie wajukuu zako.
Dada weee, wanaume nao hawapigiwi, hawajapigiwa wanacheza ukiwapigia unafikiri nini kitakachofanyika, utagombaniwa kama mpira wa kona na kujiona upo juu kumbe popo ukijisaidia unajichafua mwenyewe. Mwanaume akiwa na shida na kitu yupo radhi hata kuuza nyumba ya urithi ili tu akupate, si unalipa wakati huo.
Lakini uzuri haukai milele na mwili wa kuchezewa sana unapoteza mvuto na heshima mtaani, unajikuta ukiitwa majina ya kebehi Ooh, godoro la wanafunzi, mama huruma, jamvi la wageni au Call Box kila mwenye uwezo hujisevia.
Waswahili wanasema muda hausimami, kila uvutapo pumzi hesabu dakika inakwenda, umri unasogea uzuri nao unapotea. Pia haohao waswahili hawakukoma waliposema uanike wakati wa jua likiwa kali lakini ukicheza nalo utautwanga mbichi.
Walikuwa na maana nzito hasa kwetu wasichana kuutumia usichana wetu vizuri hasa pale tunapopata nafasi ya kutaka kuolewa kutokana na Mungu kutujalia sura na maumbile.
Kuna dada mmoja ambaye wakati sisi ndiyo tunapevuka alikuwa akitetemesha mtaa, kila mwanaume aliyemuona alitaka urafiki, wenye fedha walishindana kutangaza ndoa. Badala ya kuchagua mwanaume mmoja amuoe atulie, yeye aliona fahari kuwabadili kama nguo. Mwanaume gani hakuujua mwili wake.
Baada ya kuugawa hovyo mwili wake kila mtu alimdharau, hakuna aliyemfuata baada ya kujua ni maharage ya Mbeya. Matokeo yake akawa uwanja wa mazoezi kwa wapenda ngono, hakutofautiana na changudoa.
Baadaye aliposhtuka, alishachelewa, alitaka kuolewa lakini sifa yake mbaya hakuna mwanaume aliyejitokeza. Baada ya kujiona amedoda akawa kila siku kwa waganga kutafuta dawa ya mvuto, kweli wanaume alipata lakini hakukuwa na muoaji.
Kila siku fedha yake iliishia kwa waganga lakini sifa yake ndiyo iliyomkosesha wanaume.Nani akuoe nawe kishata mtaa? Kwa tabia hizi tutazidi kujazana mabarazani kusubiri kuchukua waume wa wenzetu.
Yangu yanatosha ujumbe umefika, ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.
GPL
3 comments:
What about wanaume nao wakimaliza mtaa mzima? A real woman won't marry THAT!!
mlay nakuunga mkono mwanamke mwenzangu what about wanaume wakimaliza mtaa mzima? ndo maana nakala hizi huwa sipendagi kusizoma sana kwa sababu anayeandika ni mwanamme na anaakili ya jinsi yake ya kiume na mtazamo wake ndo maana hapa anatuleta zake za kuleta kila saa kujidai kuwa kungwi kwa wanawake wakati hawezi kujibu jibu hilo hapo juu WHAT ABOUT WANAUME WANAOMALIZA MTAA MZIMA?
Na ni waanawake dhaifu wanaotaka kuolewa na kuteseka kwa mwanamme mwenye akili finyu wanawake waliokuwa wanajiamini wanataka kidume cha mbegu kiuhakika anajuwa kupenda kuhudumia na kujua thamani ya mwanamkee.
nimefurahi sana mlay kuweka maneno yako machache lakini ni mazito sana na nakuunga mkono sana kabisa.
tumsubiri kungwi wa kiume huyu atujibu kama ataweza
wewe si mwanamkee unajidai kujiita jina la kike nasra lakini si nasra wewe tumeshakushtukizia si mwanamke wewe ni mwanamme wewe.kuwa mkweli na muwazi.
Post a Comment