Mumewe mwanamke aliyehukumiwa
kifo nchini Suudan kwa kosa la kuasi dini ya kiisilamu, ameambia BBC
kuwa hajafahamishwa kuhusu mpango wa kumwachilia mkewe.
Ripoti zilizotolewa Jumamosi ziliarifu kwamba
afisa mmoja wa serikali alithibitisha Meriam Ibrahim, aliyejifungua mtoto akiwa kizuizini ataachiliwa katika siku chache zijazo.
Taarifa za hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mwanamke huyo, zimeikera sana jamii ya kimataifa.
Alikataa kusilimu na kusema kuwa yeye ni mkristo na hivyo anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa kwa kosa la kuasi dini.
Naibu waziri wa mambo ya nje wa Sudan, Abdullahi al-Azreg, aliambia BBC Jumamosi kwamba, Bi Ibahim ataachiliwa huru kwani serikali ya Sudan inawapa watu uhuru wa kuabudu na hivyo iko tayari kumlinda.
Mumewe Meriam Daniel Wami, alisema kuwa taarifa za mkewe kuachiliwa ambazo amezisikia kupitia vyombo vya habari, ni kama uvumi tu.
“Hakuna afisaa yeyote wa serikali amewasiliana name. Labda kuna mashauriano kati ya serikali na maafisa wa kigeni , ikiwa ni hivyo taarifa hizo mimi sina,’’ alisema Daniel.
“Mimi nitasubiri tu kesi ya rufaa ambayo mawakili wamewasilisha, na ninatamai kuwa mke wangu ataachiliwa.’’
Waziri wa mambo ya nje alifafanua kuwa Bi Meriam anaweza tu kuwa huru ikiwa mahakama itaamua hivyo katika kesi yake ya rufaa.
BBC
5 comments:
story za kutenenezwa za wana magharibi uislamu unasimama bado na wala hautetereki kwa chuki zao na njama zao watauona hivi hivi waala hawatoweza kuzima uislamu hata siku mmoja
Jamani!! Chuki gani za wanamagharibi hapa? Kwani si kweli kwamba huyu mama yupo jela? Hata Waziri wa Mambo ya Nje wa Sudan hili amelikiri. Mbona mnaingiza madai ya chuki za dini hata ambapo facts speak for themselves!! Shame on you!!
NA MUUNGA MKONO MDAU WA MWANZO NI KWELI ALIYOSEMA NA WALA HAKUNA SHAME YEYOTE ILE WATU SIKU HIZI WANATAFUTA MAMBO ILE MBAYA SI ENZI ZA ZAMANI ZA KULALA LALA OVYOO.
KUKIRI KWA HUYO WAZIRI SI HOJA SI WANANUNULIWA NA WANA MAGHARIBI TAFUTA FACT UTAONA USIWE MVIVU WA KUCHUNGUZA.
Funny! Eti uisilamu hautetereki. We are talking about someone's life here we unasema 'uisilamu hautetereki'. Who cares kama hautetereki? You can't go around killing everybody because wamekataa kuwa waisilamu. I just don't understand some people!!
funny for you the last anonymous who comment on this issue kwa sababu akili zako hazitaki kufika huko mbali alivyosema mwenzako usislamu hatetereki hujaelewa na wala hutoelewa na its true you don't care and you cant care kwa sababu akili yako hachanganyi ni kweli maisha ya mtu haya lakini who stated the PROPAGANDA ya kuwauwa watu some historia utajua, watu wanafanya mambo yao chini kwa chini halafu wanawaweka wakina mama kama hawa ETI WANATAKA KUULIWA KWA VILE HAWAUTAKII UISLAMU, WHAT A CHEAP PUBLICITY.
akii yako haifiki huko hujui dunia inavyokwenda ndo maana unaona juu kwa juu and you will never ever understand some people who are capable of using their brain very well bila ya emotions.
Post a Comment