ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, June 17, 2014

VIMINI, MGONGO WAZI MARUFUKU MAHAKAMA YA KINONDONI


Mahakama Hakimu Mkazi Kinondoni, Dar es Salaam imetoa amri ya kuzuia watu wenye mavazi yasiyo na staha kuingia makahamani hapo.
Miongoni mwa mavazi ambayo akivaa mtu anazuiwa kuingia si tu ndani ya vyumba vya Mahakama, bali pia kwenye viwanja vyake, ni yanayobana, yanayoacha mgongo wazi, nguo fupi na, mashati au blauzi za mikono mifupi.
Hatua hiyo ambayo ilianza
kutekelezwa takribani wiki tatu zilizopita inamhusu mtu yeyote mwenye shughuli mahakamani hapo wakiwemo mashahidi, wasikilizaji wa kesi na wanaohitaji huduma mbalimbali.
Akithibitisha kuhusu uamuzi huo, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Kweyi Rusemwa amesema kuwa mavazi hayo yanashusha heshima na hivyo watahakikisha wanaofika mahakamani hapo wanabadilika kimtazamo.

No comments: